Mkurugenzi
wa Kampuni ya kizalendo ya Kotes (T) Ltd, Max Komba (wapili kulia-waliosimama),
akikagua uchimbaji mtaro kwa ajili ya kutandika nyanya za mfumo wa mawasiliano
kwenye kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam, jana, kuunganisha kwenye
mkongo wa mawasiliano wa taifa. Kulia ni Mhandisi wa masuala ya ICT, Makao
Makuu ya Polisi, Mosses Maganza na watatu ni mhandisi wa Kotes (T) Ltd,
Mohamed Sibuga.
DAR ES SALAAM, Tanzania.
JESHI la Polisi nchini
limechukua hatua za kujiimarisha zaidi katika kuukabili uhalifu kisasa zaidi
kwa kuamua kuviunganisha vituo vyake vikubwa kwenye mtandao wa mawasiliano
katika mkongo wa taifa.
Kufuatia hatua hiyo,
ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano hayo ya kuunganishwa kwenye mkongo wa
taifa wa mawasiliano, umeshaanza kwenye vituo vikubwa vya polisi katika mikoa
ya Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Zanzibara na jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na
waandishi wa habari, jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kotes (T) Limited iliyopewa
na jeshi la polisi kutengeneza mindombinu hiyo, Max Komba, alisema, ujenzi huo
ulianza kwenye Kituo cha Polisi Kurasini, Chuo Cha Polisi Chang’ombe na
Oysterbay ambako ujenzi wake ulitarajiwa kukamilika jana.
Komba alisema, kampuni
yake imepewa kufanya kazi katika mikoa hiyo kwa wiki tatu, tangu ilipoanza
Julai 27 mwaka huu kwa mujibu wa mkataba, na ujenzi unatakiwa ume imekamilika
ifikapo Agosti 20 mwaka huu.
Likizungumzia mradi huo, Jeshi la Polisi
kupitia msemaji wake, lilisema, mradi huo ukikamilika utasaidia jeshi hilo
kupunguza gharama na muda mwingi ambao limekuwa
0 comments:
Post a Comment