Usaili kwa wanaoomba
kuteuliwa kuwa wagombea uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) na ule wa Bodi wa Ligi Kuu (TPL Board) unaanza leo (Agosti 30).
Kwa mujibu wa ratiba
iliyotolewa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Agosti 30 mwaka huu ni usaili kwa
waombaji uongozi wote katika Bodi ya Ligi Kuu pamoja na waombaji uongozi wa TFF
kwa kanda namba 11 (Morogoro na Pwani), kanda namba 12 (Kilimanjaro na Tanga)
na kanda namba 13 (Dar es Salaam).
Agosti 31 mwaka huu ni kanda
namba sita (Rukwa na Katavi), kanda namba saba (Mbeya na Iringa), kanda namba
nane (Njombe na Ruvuma), kanda namba tisa (Lindi na Mtwara) na kanda namba kumi
(Dodoma na Singida).
Usaili kwa kanda namba moja
(Geita na Kagera), kanda namba mbili (Mara na Mwanza), kanda namba tatu (Simiyu
na Shinyanga), kanda namba nne (Arusha na Manyara) kanda namba tano (Kigoma na
Tabora), na nafasi za Rais na Makamu wa Rais wa TFF utafanyika Septemba Mosi
mwaka huu.
Waombaji wote wamepangiwa muda wao wa
usaili. Kwa mujibu wa ratiba usaili ufanyika kuanzia saa 3 kamili asubuhi hadi
saa 2 usiku. Wasailiwa wote wanatakiwa kuzingatia muda waliopangiwa.
0 comments:
Post a Comment