ULIMWENGU umepatwa na mshtuko mkubwa kwa kuona picha
za tukio kubwa la kigaidi kwenye moja ya maduka makubwa jijini Nairobi.
Hili ni
shambulio kubwa la kigaidi kupata kutokea Afrika Mashariki tangu lile la mwaka
1998. Na ajabu ya kihitoria ni kuwa matukio mengi ya kigaidi yametokea katika
mwezi wa Septemba.
La Nairobi ni shambulizi la kigaidi la kulaaniwa
vikali na wapenda amani wote ulimwenguni. Hata hivyo, moja ya tafsiri ya
vitendo vya kigaidi tunavyovishuhudia Nairobi ni kuwepo kwa hali ya vita vya
kigaidi vyenye kuendeshwa kwenye maeneo ya mijini (Urban terrorism).
Ni shambulizi lenye athari mbaya kiuchumi si tu kwa
nchi ya Kenya, bali hata majirani zake ikiwemo Tanzania. Ni shambulizi
lililowaogopesha wageni wengi wakiwamo wawekezaji pia.
Kwamba Al Shabaab
inalenga pia nchi za Magharibi. Hivyo basi,
hata raia wake. Kunahitajika jitihada za pamoja
kuwaondoa hofu watu wa mataifa ya nje, kuwa kilichotokea Nairobi kitadhibitiwa
kwa njia zote, kisitokee tena.
Na hakika, aina hii ya ugaidi ni ngumu sana
kudhibitika hatakama nchi ina jeshi kubwa na lenye vifaa vya kisasa. Inahitaji
ushiriki wa raia wema katika kutoa taarifa za wahalifu hata kabla hawajafanya
matendo yao maovu. Inahitaji pia maandalizi makini, ya kuwa na vikosi vilivyo
tayari wakati wote kukabiliana na matukio kama haya.
Ni dhahiri, kuwa mbinu inazotumika kikundi cha kigaidi
cha Al Shaabab ambacho maana hasa ya jina hilo ni ' Vijana', ni moja ya
changamoto kubwa katika mapambano dhidi ya ugaidi.
Al Shabaab iliundwa mwaka 2006. Kinasemekana kuwa na
wapiganaji wenye silaha wapatao 10,000.
Al Shabaab katika miaka ya karibuni
wamepoteza maeneo mengi ya mijini waliyokuwa wakiyadhibiti, ikiwamo mji wa
Kismayu ambao majeshi ya Kenya yaliudhibiti baada ya kuwasambaratisha Al
Shabaab.
Kwa sasa Al Shabaab bado wana nguvu maeneo ya vijijini katika Somalia.
Kufuatia Kenya kujiingisha kijeshi kupanbana na Al
Shaabab, kikundi hicho kimeifanya Kenya kuwa adui na kutangaza wazi azma yake
ya kuishambulia Kenya.
Mwezi Aprili mwaka huu watu watano walipoteza maisha
nchini Kenya baada ya wapiganaji wa Al Shabaab kuingia kwa nguvu wakiwa na
silaha kwenye mgahawa mmoja kwenye mji wa Garissa nchini Kenya.
Mwaka 2012 ndipo Al Shabaab walipojiunga rasmi na
mtandao wa kigaidi wa Al qaida chini ya kiongozi wa Al qiada, Ayman al-
Zawahiri.
Hakika, hapa duniani matukio ya kigaidi yameongezeka.
Kwa faida ya wasomaji, nitaanza kwa kuangalia chimbuko la ugaidi kihistoria.
Kwa faida ya wasomaji, nitaanza kwa kuangalia chimbuko la ugaidi kihistoria.
Ni
rahisi kusema kwamba ulimwengu umebadilika baada ya ugaidi wa Septemba 11 mwaka
2001 kule Marekani.
Kwamba ugaidi umesogea karibu zaidi katika fikra zetu.
Watanzania bado tunakumbuka tukio la shambulizi la kigaidi dhidi ya jengo la
Ubalozi wa Marekani jijini Dar Es Salaam Agosti 7, 1998.
Sura ya ugaidi imeonekana vema zaidi miongoni mwa
walimwengu.
Bila shaka, picha ya filamu ya televisheni yenye kuonesha majengo
mawili ya World Trade Centre kule Marekani yakitunguliwa na kuanguka, zimeonwa
na takribani asilimia 75 ya watu wa ulimwengu huu. Katika hili la kuchambua
ugaidi, hebu
basi tuanze na kujiuliza;
basi tuanze na kujiuliza;
Ugaidi ni nini?
Itakumbukwa wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano
walipokutana Dodoma mwaka 2002 walipitisha Muswaada wa Ugaidi.
Wabunge wetu
walitumia muda mwingi sana kujadili tafsiri ya neno "ugaidi".
Kwa kifupi, ugaidi ukitafsiri kutoka neno la
Kiingereza "Terrorism" tunapata maana ya "hofu". Neno la
Kiingereza "Terror" lina maana ya hali ya "kutisha".
Vitendo vya kigaidi hutumiwa na mtu au makundi ya watu
ili kuwaingizia watu hofu ndani ya mioyo yao na pengine hata kuchukua madaraka
ya kisiasa.
Ugaidi ni njia ya mnyonge na hata mwenye nguvu kutimiza malengo
yake. Hili litafafanulika zaidi kadri utakapofuatilia maandiko haya.
Kihistoria tunaona kuwa, vitendo vingi vya kigaidi
humu duniani vimefanywa pia na dola zilizo madarakani kwa minajili ya kuendelea
kushika hatamu za dola.
Mathalan, msemo wa " Utawala dhalimu" kwa
tafsiri ya Kiingereza "Terror regime" hutumika tunapoielezea dola
yenye kutumia mabavu na nguvu nyingi kupita kiasi. Dola au mtawala
asiyezingatia sheria wala haki za kibinadamu.
Msamiati huu wa utawala dhalimu unatokana na lugha ya
Kifaransa na una chimbuko la Mapinduzi ya Wananchi kule Ufaransa kati ya mwaka
1789 hadi 1799.
Utawala dhalimu wenye kutisha" la terreur" ulikuwepo
kule Ufaransa kunako miaka ya kati ya 1792 hadi 1794. Katika kipindi hicho watu
takribani 40,000, wengi wao wakiwa wakulima na wahunzi waliuawa.
Mifano ya tawala dhalimu na za kutisha katika sehemu
nyingine za dunia ni kama Urusi ya zamani chini ya dikteta Stalin, utawala wa
Kinazi wa Ujerumani kati ya 1933-1945 chini ya Fashisti Hittler.
Katika Afrika, tuna pia mifano kadhaa ya tawala dhalimu
na za kutisha ambazo kimsingi ni tawala za kigaidi. Uganda ya Idd Amin, Afrika
ya Kati ya Bokassa, Zaire ya Mobutu, na nchi nyingine nyingi. Hizi zilikuwa
tawala dhalimu.
Ugaidi kimsingi ni ile hali ya mtu, kikundi au dola,
kwa maana ya taifa,kutumia nguvu nje ya wigo wa sheria ili kufikia malengo yao.
Mwenye kuendesha vitendo vya kigaidi huchagua watu wake watakaoathirika na
vitendo hivyo.
Si lazima mtu au watu hao watakaoathirika wawe ni wahusika wa
moja kwa moja wa mgogoro husika, isipokuwa, waathirika mara nyingi huchaguliwa
na huonekana kama wawakilishi wa malengo ambayo magaidi wanataka kuyafikia.
Malengo au sababu za ugaidi zaweza kuwa ni za kidini, kijamii na kisiasa.
Ugaidi huwa wa kimataifa pale tukio la kigaidi
linapofanywa nje ya mipakaya yule anayatenda tendo la kigaidi, au raia wa nchi
moja wanapokuwawalengwa na kauthirika na tendo la kigaidi katika nchi ya tatu,
mathalan,magaidi kutoka Colombia wanapofanya tendo la kigaidi dhidi ya raia
waUingereza katika nchi ya Zambia.
Source Raia Mwema.
0 comments:
Post a Comment