Image
Image

MAANDAMANO MAKUBWA YA UPINZANI TANZANIA,MBOWE,LIPUMBA, MBATIA KUWEKA HISTORIA.


Ni Prof Ibrahimu Lipumba Bingwa wa Uchumi Duniani, Freeman Mbowe Mwanasiasa Machachari, James Mbatia Mhandisi (Eng) Bahari, ndio watakao waongoza Maelfu ya Watanzani katika MANDAMANO Makubwa na kuandika Historia ya UKOMBOZI wa TAIFA hili,

Yale Maandamano makubwa na ya Kihistoria ndiyo yameshafika muda wake.
Ni siku ya Jumamosi Tarehe 21 Septemba,2013 kuanzia saa 3 Asubuhi mambo yataanzia katika Makutano ya Barabara za Pugu na Mandela Road eneo la Tazara.

Maandamano hayo ambayo yataongozwa na Viongozi wakuu wa vyama vya CUF,NCCR na Chadema,yatapitia Buguruni Sheli - Ilala Boma - Kariakoo Uhuru - Msimbazi - Fire na kuishia katika Viwanja vya Jangwani ambapo

Wanachama,wakiongozwa na Mwenyeviti wao Prof.Ibrahim lipumba:The Creative economist of Africa Freeman Mbowe Mzee wa Helkopta , James Mbatia Mhandisi (Eng) Bahari watahutubia Mamia Elfu ya wananchi watakaojitokeza.

RATIBA YA MIKUTANO YA VIONGOZI WA CUF,CHADEMA NA NCCR Katika kupigania KATIBA MPYA YA WATANZANIA ni kama ifuatavyo;
1. Jumamosi tarehe 21 Septemba,2013 - Dar es Salaam Jangwani.
2. Jumapili tarehe 22 Septemba 2013 - Mwanza
3. Jumatatu tarehe 23 Septemba 2013 Kigoma
4. Jumanne tarehe 24 Septemba 2013 Arusha na
5. Jumatano tarehe 25 Septemba 2013 Balaa litakuwa Zanzibar

"TUNAANZA NA DAR,MIKOANI WANAMALIZIA"
"ASIBAKI MTU NYUMBANI,TUKAPIGANIE KATIBA YA WATANZANIA"

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment