Bondia
Francis Cheka akiwa sambamba na Mkanda wake aliokabidhiwa Agost 30 baada ya
kumtwanga Mmarekani Phil William mwishoni mwa wiki ndani ya ukumbi wa
Diamond Jubilee jijini Dar,na hapo bondia huyo akionekana akiwa na
mashabiki wake wakati alipokuwa akiwasili mkoani Morogoro anakoishi.
Jimmy Mengel,Morogoro.
Mamia ya wakazi wa manispaa ya
Morogoro wamekunyika kumpokea bingwa wa ngumi
duniani (WBF) Francis Cheka aliyewasili mkoani humo siku chache baada ya
kumtwanga Mmarekani Phill Williams Ijumaa iliyopita Jijini Dar es Salaam na
kutwaa mkanda huo wa ngumi duniani.
Wakazi hao wa Morogoro wamempokea shujaa
huyo kwa maandano yaliyozunguka kwenye mji huo Morogoro na kuishia kwenye
Ukukbi wa Old Trafford ambako wananchi pamoja na viongozi mbalimbalio
walijumuika pamoja na kumpongeza nyota huyo.
Aidha kwa upande bingwa huyo wa dunia
licha ya kusifu kiwango kilichoonyeshwa na mpinzani wake,amewashukuru
watanzania waliojitokeza kumuunga mkono
kabla wakati na baada ya pambano hilo la dunia.
Akizungumzia pambano hilo kocha wa bondia huyo Salehe Komando amesema lilikuwa zuri na kwamba ushindi wa Cheka umetokana na jitihada zake na hivyo
anajiandaa kwenda Afrika Kusini kunolewa zaidi ikiwa ni pamoja na kuandaliwa
pambano mjini Morogoro Mkuu wa Wilaya ya Morohoro Said Amanzi akiahidi
kushirikiana na bondia huyo ili aweze kutimiza malengo yake.
Wakati huo huo Wadau mbalimbali wa
michezo akiwemo Waziri wa Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi Dk.David Mathayo amewataka waandaaji mapambano ya ngumi
nchini kuacha ubabaishaji ili kujenga imani kwa wananchi na huku akizungumzia
tukio la bondia huyo wa marekani ya kukataa kupanda uliongoni hadi alipwe
kwanza fedha zake shilingi milioni 12 kuwa ni tukio la aibu kwa taifa na kwa
wanamichezo kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment