Wananchi wa Japan
wanaendelea kusherehekea nchi hiyo kuchaguliwa kuwa wenyeji wa michezo ya
majira ya kiangazi ya Olimpiki ya mwaka 2020.
Nchi hiyo ilipata
nafasi hiyo baada ya kuishinda miji ya Madrid na Intabul katika kinyang'anyiro
hicho.
Baadhi ya wananchi wa
nchi hiyo wameielezea fursa hiyo kuwa pamoja na mambo mengine ikiwemo faida za
kiuchumi, itawaleta pamoja Wajapani waliokumbwa
na majanga ikiwemo ya Tsunami mwaka 2011 na mlipuko wa kinu cha Nyuklia
cha Fukushima.
Awali waziri mkuu wa
nchi hito Sinzo Abe,alihakikishia jumuia ya kimataifa kuwa hali ya mambo
itakuwa sawa licha ya kuvuja kwa kinu hicho cha nyuklia.
0 comments:
Post a Comment