Akizungumza katika
mahojiano na Kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Runinga ya East Africa chini ya
Mtangazaji, Salama Jabiri mwanzoni mwa wiki hii, Gurumo alisema miongoni mwa
mambo mabaya ambayo hawezi kuyasahau maishani mwake ni pamoja na hayo.
KUFUMANIWA:
Katika sakata hilo,
Gurumo alisema kuwa ilikuwa ni mwaka 1961 ambapo alikuwa na uhusiano na mke wa
mtu ambaye aligoma kumtaja, ndipo siku moja wakiwa nyumbani kwa mwanamke huyo
‘wakiponda kirauli’ ghafla walisikia hodi na ndipo mwanamke huyo alipomwambia
kuwa anayegonga mlango ni mumewe.
“Niliogopa sana,
ikabidi nijibanze nyuma ya mlango, alipoingia tu nikatimua mbio kali sana,
lakini hakujua kama ni mimi,” alisema Gurumo.
Kuhusu uvutaji wa
bangi, Gurumo alikiri kuwahi kuonja kilevi hicho ujanani mwake ambapo
alibainisha kuwa alishawishiwa na mwimbaji mwenzake maarufu sana kwa wakati
huo.
Alisema siku ambayo
alivuta sigara kubwa, alipofika nyumbani baada ya kutengewa chakula, alimega
ugali na kuchovya kwenye maji ya kunawa akidhani ni mchuzi.
“Siku hiyo ilikuwa
mbaya sana kwangu, nilivuta kutokana na ushawishi, baada ya kufika nyumbani,
wakati wa chakula nilimega ugali na kuchovya kwenye maji ya kunawa, nikasema
mbona mchuzi hauna ladha nzuri, lakini baadaye nilijutia sana,” alisema Gurumo
na kuongeza:
“Nimepitia maisha
ambayo si mazuri sana ujanani, lakini yote hayo ni mapito na imebaki kama
historia tu kwangu, namuomba Mungu anisamehe kwa hayo,” alisema Gurumo.
0 comments:
Post a Comment