Mchungaji Kadani Limbu ambaye ni Katibu wa Kanisa la EAGT Makao Makuu
(Ujenzi) akisoma wasifu wa marehemu Askofu Kulola aliyezaliwa 1928 katika
Kijiji cha Nyang’honge Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza na kujaliwa kupata elimu
ya msingi (Middle School) na sekondari ya Bwiru Boys Mwanza kati ya mwaka 1946
hadi 1949 kuendelea na masomo na kupata Civil Technician.
Baada ya kumaliza na kupata utaalamu huo na kuajiliwa kuwa mtumishi wa
serikali katika Halmashauri ya Mji wa Mwanza kama Mhandisi wa Mchoraji wa
Ramani za majengo na Barabara wakati wa uhai wake aliamua kuacha kazi na kuanza
utumishi wa mungu akifanya kazi kwa kutembea kila mahali akihubiri Injili kwa
watu mbalimbali.
Wasifu huo ulimwelezea Askofu Kulola wakati wa utumishi wake wa kiroho
kuwa alikuwa akitembea kwa miguu kuanzia mwaka 1962 akihubiri neno la
Mungu .Baada ya kuacha kazi za serikali mwaka 1951 alipatwa na matatizo na
kuwahi kufungwa gerezani na kupigwa na bwana jela na kuumizwa vibaya muguu wake
wa kushoto na kupelekea kupata kilema ambapo aliwekewa mguu wa bandia.
Marehemu Askofu Kulola ameacha mke na watoto 10 wajukuu 42 vitukuu 16 na
amekuwa mutumishi wa kiroho tangu akiwa na umri wa miaka 18..
0 comments:
Post a Comment