KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
“PRESS RELEASE” TAREHE 23. 10. 2013.
WILAYA YA MBARALI – AJALI YA PIKIPIKI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.
MNAMO TAREHE 22.10.2013 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MKOMBWE, KATA YA UBARUKU, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. PIKIPIKI T.656 BDG AINA YA LIFAN IKIENDESHWA NA WAKATI S/O CHARLES, MIAKA 22, MBUNGU, MKAZI WA MKOMBWE, LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO AGREY S/O MPWEPWA, MIAKA 5, MSANGU, MKAZI WA KIJIJI CHA MKOMBWE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA MISHENI RUJEWA AMBAYE MWILI WAKE UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. AIDHA KATIKA AJALI HIYO MWENDESHA PIKIPIKI ALIJERUHIWA NA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI HIYO, TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI KUGONGA GARI NYINGINE KWA NYUMA NA
KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.
MNAMO TAREHE 22.10.2013 SAA 19:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MACHIMBO, KATA YA UJELELE, TARAFA YA RUJEWA, BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI T.964 AUN/T.730 BPL AINA YA SCANIA TANKI LIKIENDESHWA NA DEREVA SAMORA S/O PETER, MIAKA 35, MHEHE, MKAZI WA DSM, LILIGONGA KWA NYUMA GARI T.641 AQQ/ T.935 AUV AINA YA SCANIA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALLY S/O SALIM, MIAKA 38, MPARE MKAZI WA DSM NA KUSABABISHA KIFO UTINGO WA GARI T.964 AUN/T.730 BPL ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA HAMAD S/O ? NA MAJERUHI KWA DEREVA SAMORA S/O PETER AMBAYE AMELAZWA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA, TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI T.964 AUN/T.730 BPL. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI
MNAMO TAREHE 22.10.2013 MAJIRA YA SAA 05:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA BITIMANYANGA, KATA YA MAFYEKO , TARAFA YAKIPEMBAWE WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA KILINGO S/O FURAHISHA, MIAKA 36, MKIMBU, MKULIMA, MKAZI WA BITIMANYANGA AKIWA NA NYARA ZA SERIKALI KILO KUMI [10] ZA NYAMA YA TWIGA. MTUHUMIWA NI MUWINDAJI HARAMU. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI NYARA ZA SERIKALI ISIVYO HALALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/WATU/KIKUNDI KINACHOFANYA SHUGHULI ZA UWINDAJI HARAMU AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAHUSIKA WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment