Mshiriki Joshua Kahoza
akiimba wakati wa mkutano na waandishi wa
habari,Anayetazama kushoto ni
Mtaalamu wa Huduma za Ziada wa Zantel,
Cecil Muhina, na jaji mkuu wa Epiq BSS,
Ritha Paulsen.
Jaji Mkuu wa Epiq BSS,
Ritha Paulsen, akizungumza na waandishi wa
habari leo kuhusiana na maenedeleo
ya kipindi hicho,Kulia kwake ni Haji
Yussuf, Meneja Huduma za ziada, na kushoto
ni Mtaalamu wa huduma za
ziada, Cecil Muhina.
Mshiriki First Godfrey
akiimba mbele ya waandishi wa habari.
Anayetazama kushoto ni Mtaalamu wa
Huduma za Ziada wa Zantel, Cecil
Muhina, na jaji mkuu wa Epiq BSS, Ritha
Paulsen, mwisho ni Haji Yussuf,
Meneja Huduma za Ziada.
Mshiriki
Elizabeth Mwaakijambile akitoa burudani kwa waandishi wa habari leo.
Anayetazama kushoto ni Mtaalamu wa Huduma za Ziada wa Zantel, Cecil Muhina, na
jaji mkuu wa Epiq BSS, Ritha Paulsen.
Na.Mwandishi wetu.
Shindano la kumtafuta mkali wa kuimba katika miondoko ya Bongo flava Epiq BSS limeingia katika hatua za mwisho wiki hii likiwa
limebakiza washiriki kumi na mbili, kuelekea kumpata mshindi wa shilingi
milioni hamsini pamoja na mkataba wa kurekodi.
Washiriki waliochaguliwa kwa usaili wa simu, nao waliungana na wenzao
waliongia kumi bora wiki hii na konyesha uwezo mkubwa, hali inayoashiria
kutakuwa na kazi kubwa kumchagua mshindi.
Washiriki waliobaki
mpaka sasa na namba zao za ushiriki ni Amina Chibaba (03), Elizabeth
Mwakijambile (08), Emmanuel Msuya (21), First Godfrey (11), Francis Flavian
(09), Furaha Charles (14), Furaha Mkwama (06), Joshua Kahoza (02), Maina Thadei
(5), Mandela Nicholas (10), Melisa John (22) na Raymond John (23).
Akizungumzia hatua ambayo shindano limefikia, jaji mkuu wa shidano hilo,
Ritha Paulsen, aliwataka wananchi watumie vema nafasi ya kupiga kura kwa
kuchagua washiriki wenye vipaji vikubwa.
‘Hatua hii ni muhimu
sana, hasa kwa kuwa inalirudisha shindano kwa wananchi ili waweze kumchagua
mshindi wao, hivyo nawaomba wawapigie kura kwa wingi’ alisema Ritha.
Akizungumzia ubora wa washiriki wa mwaka huu, Ritha alisema wamepata
washiriki bora zaidi, na pia mafunzo wanayoyapata ndani ya jumba la Epiq BSS ni
makubwa hivyo mashabiki watarajie mchuano mkubwa zaidi katika kuwania milioni
hamsini.
Kwa upande wake Afsa Biashara Mkuu wa Zantel,
Sajid Khan, amewataka wananchi wawapigie kura washiriki wanaoamini ni wazuri na
watafanya vizuri kwenye soko.
‘Maana ya kufungua laini za watu kupiga kura
mapema ni kuwapa nafasi ya kuchagua mshindi wanayempenda’ alisema Khan.
Kampuni ya Zantel pia imerahisisha namna ya upigaji kura kwa kutoa namba
maalumu ya kupiga kura kwa kupiga simu namba 0901551000, na kwa njia ya ujumbe
mfupi mashabiki wa Epiq BSS wataweza kuwapigia washiriki wanaowapenda kwa
kuandika neno KURA, halafu waache nafasi, namba ya mshiriki halafu watume kwenda
15530.
0 comments:
Post a Comment