Image
Image

NCHIMBI KUFUNGUA MKUTANO WA JESHI LA MAGEREZA OCKTOBA 24 MWAKA MKOANI MOROP GORO.



Waziri wa Mambo yaNdaniyaNchiDkt.EmmanuelNchimbianatarajia kufungua mkutano wa siku mbili wa Maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza utakaofanyika kuanzia Oktoba 24, mwaka huu mkoani Morogoro.

Mkutano huo ndiyo mkutano wa juu kabisa katika jeshi la Magereza ambao uwahusisha wakuu wa Magereza wa Mikoa ya kiutawala Nchini, Maafisa waandamizi toka Makao Makuu pamoja na Wakuu wa Taasisi sita za ndani ya jeshi la Magereza ambazo kimuundo wa utawala zina hadhi ya mikoa.

Taasisi hizo ni pamoja na Chuo cha maafisa Ukonga mkoani Dar es Salaam, Chuo cha mafunzo ya awali Kiwira Mkoani Mbeya, chuo cha Ufundi Ruanda Mbeya, chuo cha Udereva na ufundi mitambo cha Kingilwira mkoani morogoro, kikosi Maalum cha kutuliza ghasia Magerezani Ukonga Dar es Salaam pamoja na Shule ya Sekondari Bwawani iliyoko mkoani Pwani.

Aidha  kwa mujibu wa taarifa  iliyotolewa kwa vyombo vya habari na   Kamishna  Jenerali  wa Magereza  Juma Mlewa  inasema kuwa madhumuni ya mkutano huo wa kila mwaka ni kutathmini kwa pamoja utendaji wa jeshi hilo katika maeneo yake yote na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizopo pamoja na kurekebisha dosari zilizojitokeza na kuweka malengo ya kuboresha utendaji kazi katika mwaka unaofuata.

Mkutano huo, ambao mada kuu itakuwa ni utendaji kazi wa kasi na tija kwa matokeo makubwa sasa pia watazungumzia fursa mbalimbali za kuwezesha jeshi  hilo  kujitegemea, mpango wa uchangiaji wa hiari Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) pamoja na mada ya urekebishaji wafungwa itakayotolewa  na Makao makuu ya Magereza.

Mkutano huo unatarajiwa kufungwa na kamishna Jenerali wa Magereza John Minja.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment