Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.
Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius
Nyaisangah Katika viwanja vya leaders Club Jijini Dar es Salaam,(Picha Na
Semvua Msangi Tambarare Halisi).
Na. Semvua Msangi,Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Mohammed
Gharib Billal, Amewaongoza watanzania Katika kuuga na kutoa Heshima za
Mwisho katika Msiba wa Mtangazaji na
Mwandishi wa Habari Julius
Nyaisangah Katika Viwanja vya Leaders Jjijini Dar es Salaam.
Licha ya kuwaongoza wananchi katika kuuaga mwili huo Pia
alikuwepo kiongozi wa wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Makampuni ya IPP
Media Regnal Mengi Sambamba na Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri nchini
Tanzania Absalum Kibabanda.
Dk Bilall alisema kuwa Kifo cha Mtangazaji huyo wamekipokea kwa Huzuni kubwa Kama serikali kwani
alikuwa ni Mtangazaji ambaye alikuwa anafanya kazi kwa kuzingatia maadili ya
utangazaji na kuongea kitu ambacho kilikuwa kinamantiki na mashiko kwa jamii
licha ya kuwa alifanya kazi kipindi ambacho viombo vya Habari vilikuwa vichache
na hivyo kumpelekea ugumu katika ufanyaji wake wa kazi ,lakini wao kama
serikali watamkubuka Daima kwani Kazi ya Mungu Haina Makosa na Huko ndiko Kila
mja atakapo enda na kifo hakikwepeki kikubwa ni kumuombea dua afike salama Huko
aendako.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na
Maendeleo chadema Freeman Mbowe alisema
kuwa msiba nikitu ambacho huwa kila mtu kitamkuta, nakusema kuwa wanahabari ni
watu makini mno hasa katika kuandika habari zao lakini akasisitiza kuwa kuwepo
wa utamaduni wa wanahabari kuandika
vitabu kwa lengo la kuwa na historia mbali mbali kwa vizazi vya sasa na vijavyo
kusudi kuweza kuwa tambua watu Maarufu
na wasio Maarufu kwa kupitia Historia.
Wakati nilipo muuliza swali kwanini Wanahabari Hawana Desturi
za Kuwa na utamaduni wa kuandika Historia mbali mbali katika uandishi wao, Alisema
kuwa ni mfumo wa elimu wanchi yetu na endapo utarekebishwa na kukaa sawa Basi
wanahabari watakuwa ni chachu ya kuandika historia kwa kuacha kumbu kumbu ya
vitabu na hata vyuo vinavyo fundisha Taaluma hii ya Habari.
Naye Mwenyekiti wa jukwaa la Wahariri absalum Kibanda alisema
kuwa julias nyaisangah alikuwa mwalimu na kiongozi wa wanahabari, na amekuwa
akiwatia hamasa wanahabari hata
walipokuwa katika shughuli zao huko mikoani, kwani nyaisangah hakuwa mbaguzi
alikuwa ni mchangamfu na alikuwa mtu wa watu kwahiyo wao kama wanahabari watamkumbuka
zaidi na zaidi katika taaluma hii kwani pengo lake nikubwa na hakuna
wakuliziba.
Pia Meneja Matangazo wa Abood Media, Abeid dogoli akizungumza
kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Abood Media, Abdulazizi Mohamed Abood alimzungumzia marehemu nyaisangah kutokana na
ni mtu ambaye wamekuwa wakifanya naye kazi bega kwa bega hadi siku ya mwisho na
kusema kuwa, wao kama abood media wamepata pengo kubwa kwa mtu ambaye alikuwa
anaweza kuelekeza watu katika tasnia hii ya habari na mtu ambaye alikuwa mahiri, lakini walijitahidi kwa kila namna
kumuokoa maisha yake lakini kama ilivyo kuwa mungu akimuhitaji mja wake
humchukua ndivyo ilivyokuwa hadi leo hii hatunaye Marehemu nyaisangah.
Hata hivyo mwenyekiti wa makampuni ya IPP MEDEDIA Regnal
Mengi alisema kuwa marehemu nyaisangah ni mfano wa kuigwa kwani alikuwa
mtangazaji ambaye hakuwa na majivuno mengi licha ya kuwa maarufu na mtu ambaye
alikuwa kipenzi cha wengi katika sehemu zakazi, na ndio maana ataendelea
kumkumbuka kwa yale aliyo yafanya na kuwataka wanahabari kuiga mfano wake,
licha ya kuwa tayari wapo ambao wanafuata nyendo zake kila uchao.
Aidha Marehemu alianza elimu yake ya msingi nchini Kenya
Mwanzoni mwa miaka ya 70 baada ya kumaliza alirudi nchini Tanzania na Kuanza
elimu yake ya sekondari Buhemba Tarime,Alijiunga na chuo cha utangazaji nyegezi
mwanza na kuhitimu mafunzo yake mwaka 1979 alirudi nchini Kenya na kujiunga na
shirika la Utangazaji la Kenya KBC
wakati huo ikijulikana kama Voice of Kenya kama mtangazaji.
Sasa baada ya kufanya kazi kwa Takribani mwaka mmoja Voice of
Kenya, marehemu nyaisangah alirejea nchini na kujiunga na Radio Tanzania Dar es
Salaam (RTD) Hadi mwaka 1994 na Hatimaye kujiunga na Radio One Sterio/ ITV,
alifanyakazi katika kituo hicho cha Radio one/ Itv hadi mwaka 2008 na kuhamia Radio DW ya ujerumani.
Mwaka 2010 nyaisangah alihamia Morogoro na kuanza kazi Abood
Media Kama Meneja wa kituo hicho mpaka alipofikwa na umauti tarehe 20/10/2013 katika
Hospitali ya Mazimbu Mnispaa ya Morogoro.
Marehemu nyaisangah alianza kuugua ugonjwa wa kisukari Mapema
mwaka huu, Ameacha mjane Leah julius Nyaisanga,
na watoto watatu, Samweli julius nyaisangah, Noela julius nyaisanga na
Beatres Julius Nyaisangah, amefariki akiwa na umri wa Miaka 53, amezaliwa 01
january 1960 huko Tarime Mara Na Maziko yatafanyika huko.
0 comments:
Post a Comment