udumia watu wasiojiweza.
Raia hao wa
Uingereza, Kirstie Trup na Katie Gee, hivi sasa wanaendelea kupata matibabu
katika Hospitali za Chelsea na Westminster London na taarifa zinaeleza kuwa
afya zao zimeimarika kwa kiwango cha kuridhisha hasa baada ya kufanyiwa
upasuaji na kisha kuwekewa ngozi upya.
Pamoja na madhara
waliyokumbana nayo raia hao wamesema kuwa bado hawajakatishwa tamaa na tukio
hilo na sasa wanapanga kurejea tena visiwani humo kuendelea na kile
walichokiita ‘kazi za upendo’.
Katika waraka wake
uliochapishwa na Gazeti na Daily Telegraph, Kirstie Trup amesema kuwa yeye na
mwenzake wamepanga kurejea Zanzibar mwaka ujao na kwamba safari hii wataongeza
kasi ya kushiriki kazi za kujitolea.
“Kwa sasa tuko
imara na mwakani tumepanga kurejea tena visiwani Zanzibar kushiriki katika kazi
za kujitolea,” alisema Trup ambaye ngozi yake imefanyiwa ukarabati wa kisayansi
na kuwekewa ngozi upya katika eneo la mkono wa kulia na sehemu ya bega.
Akielezea zaidi
kuhusiana na tukio hilo la kumwagiwa tindikali, Trup alisema kuwa anachokumbuka
ni kuwa wakati akiwa na mwenzie wakielekea mgahawani ghafla walijitokeza watu
wawaili na walipowakaribia walichomoa kopo kutoka kwenye mfuko na kumwaga kitu
cha majimaji ambacho baadaye kilibainika kuwa ni tindikali.
“Mwili mzima
uliwaka kama vile nimechomwa na moto. Maumivu yalikuwa makali sana yasiyoweza
kuelezeka hasa katika eneo la bega langu la kulia. Nachokumbuka kingine ni kuwa
tulipiga kelele kwa sauti sana hata kufanya wale waliokuwa kwenye hoteli
iliyokuwa jirani na sisi kutahamaki,” alisema Trup.
Amesema kuwa baada ya tukio
hilo alijitokeza mtalii ambaye aliwapa msaada kwa kuwamwagia maji sehemu
walizojeruhiwa na baada ya hapo walijitosa baharini katika kile walichoeleza ni
kujaribu kutuliza maumivu.


0 comments:
Post a Comment