Viongozi wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) wanakutana leo mjini Kampala, Uganda kujadili shirikisho la
kisiasa la kikanda, kuzindua utoaji wa viza moja kwa watalii wanaotembelea nchi
hizo na utumiaji wa vitambulisho vya taifa kwa ajili ya kusafiria kwa raia wa
nchi hizo.
Habari zinasema kuwa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na
mwenzake wa Burundi Pierre Nkurunzinza pia wamealikwa katika mkutano huo wa
Kampala.
Viongozi hao wawili hawakushiriki katika mkutano uliopita wa
viongozi wa nchi za wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika
mjini Kigali.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda imetangaza kuwa kualikwa kwa marais wa
Tanzania na Burundi ni ishara kuwa mipango hiyo inayojadiliwa inafanyika kwa
nia njema kwa ajili ya kuimarisha utangamano wa nchi za kanda hiyo.
Premi Kibanga ambaye ni Mwandishi
wa Habari wa Rais wa Rais Kikwete wa Tanzania amesema kiongozi huyo
anayejitayarisha kwa mkutano wa katiba mpya jijini Dodoma wiki ijayo atamtuma
makamu wake Dr Gharib Bilal katika mkutano wa Kampala.
Kikwete hakualikwa katika mkutano uliopita wa viongozi wa Afrika
Mashariki uliofanyika Kigali, Rwanda.
0 comments:
Post a Comment