Ban Ki-moon
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon ametoa wito wa juhudi za kufufua eneo la Afrika magharibi ambalo limeshuhudia madhara makubwa ya mlipuko wa Ebola katika historia ya dunia.
Akizungumza baada ya kukamilisha ziara yake katika nchi za Guinea, Mali, Sierra Leone na Ghana, Bw. Ban amesema ameshuhudia maendeleo yaliyofikiwa na kuongeza kuwa kiwango cha maambukizi kimepungua katika maeneo mengi. Bw Ban pia amesisitiza Umoja huo utaendelea kutoa msaada kadri mlipuko huo unavyozidi kuongezeka.
Pia amelitaka shirika la Maendeleo la Umoja huo UNDP kufanya juhudi za kufufua eneo hilo la Afrika magharibi kwa kuhakikisha kuwa huduma muhimu zinarejeshwa, watoto wanarudi shule, watu wanarudi kazini, kujenga uchumi ulioharibika na kuwahudumia watoto yatima.
Bw. Ban pia amesema jumuiya ya kimataifa inahitaji kuchukua tahadhari mapema na kujibu kwa haraka.
0 comments:
Post a Comment