Mwenyekiti wa timu ya magari
ya Ferrari Sergio Marchionne amesema anahisi msimu wa mwaka 2015 utakua mgumu.
Sergio Marchionne anapatwa na wasiwasi huku timu ya Ferrari ikiwa imemtimua
mkuu wa timu Marco Mattiacci, na kumkabidhi majukumu Maurizio Arrivabene, kuwa
kiongozi mpya.
Pia kuna mabadiliko kwa upande wa madereva ambapo Sebastian
Vettel, ndie atakua dereva kinara baada ya Fernando Alonso, kutimkia timu ya
McLaren. Hata hivyo Marchionne anaamini ujasiri unaweza kuwaokoa kupambana na
wapinzani wao haswa timu ya Mercedes.
Timu ya Ferrari haikufanya vizuri katika
msimu wa mwaka 2014.
0 comments:
Post a Comment