Nagu awataka watanzania kuwa na tabia ya kujiunga na vyama vya Ushirika.
Dk Mary Nagu
Watanzania wametakiwa kujiunga na vyama vya ushirika vya kuweka na kukopa (Saccos) kwani vinaweza kuwakwamua kiuchumi, iwapo watachagua miradi yenye faida wanapofanya biashara.
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk Mary Nagu, kuanzishwa kwa saccos hiyo ni jambo jema na la kupongezwa, kwani Watanzania wamejaliwa kuwa na rasilimali, ambapo wakiungana na kuzitumia zinaweza kuwaondoa kwenye umasikini.
Amesema vyama hivyo ni njia madhubuti ya kujikwamua kimaisha, endapo wataongozwa na watu mahiri wanaojali maslahi ya wenzao badala ya maslahi yao binafsi.
Alitoa wito kwa viongozi wa chama kilichozinduliwa kuwa na nidhamu ya kutunza fedha za wanachama wake ili waweze kufika wanakotaka na kwamba bila usimamizi madhubuti, hawawezi kufikia malengo yao na badala yake wataanguka.
0 comments:
Post a Comment