Akiwa ameketi dawati la mbele kabisa darasani
,yuko darasa la tano na amevalia nguo za shule , Priscilla Gogo Sitienei
anamsikiliza mwalimu anayefundisha kwa makini hukua akiandika majina ya wanyama
kwa kiingereza kwenye daftari lake.
Prissilla alijiunga na shule hii ya 'Leaders
Vision Preparatory School' miaka mitano iliyopita lakini pia aliwahi
kuwahudumia wakaazi wa kijiji chake cha Ndalat kilichoko kwenye bonde la ufa
kama mkunga miaka sitini na mitano iliyopita.
Darasani Priscilla anawasaidia wengine
wafanye vyema ambao wana umri kati ya miaka 10 hadi 14 na mar azote huwaambia
ujumbe wake hasa mabinti kuwa elimu ndiyo urithi wao.
Priscilla anajulikana kama Gogo maana yake
bibi katika lugha ya jamii ya wakalenjini,anasefurahia masomo akiwa na umri wa
miaka 90 katika umri huo anajua kuandika na kusoma pia fursa aliyoikosa
alipokuwa mdogo.
Lugha ambayo Priscilla anajiona yuko huru
kuitumia ni lugha mama kwake ki Kalenjin kuliko kiingereza,pindi anapotakiwa
kujieleza kwanini aliamua kujiunga na shule katika umri wake.
Sababu kubwa ambayo amekuwa akiitoa,ni ajue
kusoma ili amudu kusoma bibilia,lakini pia kwa umri wake anataka awahamasishe
watoto kupata elimu,kwani anawaona watoto wengi wakiwa hawako shuleni na watoto
hao wana watoto.
Gogo apitapo mitaani haoni shida kukabiliana
na watoto ambao hawako shuleni katika muda wa masomo na kuwauliza kwanini
hawako shuleni.
Gogo anasema watoto hao humjibu kwamba
hawaendi shule kwakuwa umri wao ni mkubwa,name huwaambia mimi ni mkubwa sana
kwenu lakini niko shuleni hivyo nanyi jiungeni na shule.
Kikubwa kinachomuumiza Gogo ni kuwaona watoto
wengi waliopoteza muelekeo,wengi wao hawana baba na wanazurura hovyo
mitaani,bila msaada wowote.kutokana na hali hiyo nataka kuwahamsisha waende
shuleni.
BBC
0 comments:
Post a Comment