Kwa habari ambazo zimefikia
Tambarare halisi muda zinasema kuwa
nyumba kadhaa zimezolewa na maji na kusababisha mafuriko mtwara mjini na
kusababisha maafaa na kuharibu miundombinu mbali mbali kufuatia mvua kubwa
iliyonyesha mkoani humo.
Kufuatia maafa hayo, Kamati ya Ulinzi na Usalalama ya mkoa wa Mtwara imeanza thathmini ya athari ya mvua hizo zilizoanza kunyesha kuanzia alfajiri ya leo.
Kufuatia maafa hayo, Kamati ya Ulinzi na Usalalama ya mkoa wa Mtwara imeanza thathmini ya athari ya mvua hizo zilizoanza kunyesha kuanzia alfajiri ya leo.
Wakati huo huo Waziri Mkuu Mheshimiwa MIZENGO PINDA anatarajiwa
kuwasili Mtwara kutembelea eneo la Msimbati wilaya ya Mtwara Vijijini kujionea
uharibifu uli o tokana na ongezeko la
kina cha maji ya bahari
kilichosababisha kumezwa kwa sehemu ya
ardhi yenye ukubwa wa mita mia moja na
sita .
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara HALIMA DENDEGU amesema mara atakapowasili
Mheshimiwa PINDA ataelekea eneo la Msimbati ambalo liko kilomita 60 kutoka
mtwara mjini.
Kuhusu maendeleo ya kudhibiti kingo za maji ya bahari Mkuu huyo wa
mkoa amesema kazi hiyo inaendelea vizuri ingawa ni ngumu kutokana na maji hayo
kuhamia sehemu nyingine na kufanya uharibifu.
Hata hivyo amesema sehemu kubwa ya kingo za bahari zimefanikiwa
kujazwa mawe na mchanga kwa wingi hatua ambayo ni ya awali ili kudhibiti mvua
kubwa ambazo zilitabiriwa na mamlaka ya hali ya hewa ya kuwapo kwa mvua kubwa
katika mikoa ya kusini siku ya leo.
0 comments:
Post a Comment