Image
Image

Mfumo wa kikoloni unao tumiwa na jeshi la polisi nchini tanzania ndio unaokiuka haki za binadamu




Serikali nchini Tanzania  imetakiwa kubadili mfumo wa utendaji Kazi  wa jeshi la polisi  kutokana na kuwa na mifumo ya kikoloni na ukandamizaji jambo linalolifanya jeshi hilo kutenda shughuli zake kwa kukiuka haki za binadamu.

Kauli hiyo imetolewa leo Tarehe 29  bungeni mjini Dodoma na baadhi ya wabunge wakati walipokuwa  wakichanga mjadala wa hoja ya Dharura ambayo  iliwasilishwa bungeni na Mh. James Mbatia kufuatia tukio la kupigwa kwa mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Pof.Lipumba wakati wa mkutano na wananchi na wanachama wa chama hicho katika kumbu kumbu ya kuwakumbuka wenzao waliokuwa wamefariki Dunia Pemba mwaka 2001.

Hata hivyo nao  baadhi ya wabunge wamemtaka waziri mkuu kuliomba bunge radhi pamoja na watanzania wote na kisha kufuta kauli yake aliyoitoa bungeni siku za nyumba isemayo (WAPIGWE TU) inayodaiwa kuhamasisha polisi kupiga raia sambamba na waziri wa mambo ya ndani Mh. Mathias  Chikawe kujiuzulu nafasi yake kufuatia kauli yake wakati wa kuwasilisha maelezo juu ya hoja ya dharura ya kupigwa mwenyekiti wa CUF.Prof  Lipumba.

Pia wamependekeza kuwajibishwa kwa baadhi ya polisi waandamizi walioshiriki katika matukio mbalimbali yaliyosababisha mauaji na majeraha kwa wananchi badala ya kuwapandisha vyeo pamoja na kuweka mifumo itakayolifanya jeshi hilo kuwa huru badala ya kuwa jeshi la kupokea maagizo.

Chikawe:"Kufatia hoja ya Mh James Mbatia Mbunge ninamaelezo yafatayo, Tar 26 Jan Jeshi la polisi lilipokea barua kutoka Chama cha CUF. Barua hiyo ilikuwa ikitoa taarifa za kufanyika kwa maandamano kwenye viwanja vya Zackiem Mbagala. 
Maandamano yalipangwa kuanzia Temeke kuelekea Zackiem, Jashi la polisi liliwaita viongozi wa CUF kwa mazungumzo. Walifanya mazungumzo na jeshi la polisi lilitoa tahadhari kadhaa kutokana na sababu za kiusalama. Viongozi wa CUF waliridhika na ushauri wa kamanda SIRO.
Katika hali ya kushangaza Profesa Ibrahimu Lipumba alikaidi Zuio la Jeshi la polisi na Kuamrisha wananchi kuandamana kuelekea Zackiem. 
Jeshi la polisi linataka kila mtu kutii sheria bila shuruti, Na mtu yoyote akishindwa kufanya hivyo jeshi la polisi litashughulikia mtu yoyote bila kujali umri, jinsia, wala madaraka yake.

Kauli hiyo ya chikawe ndiyo iliyofanya bunge kufukuta zaidi na kutakiwa kujiuzulu kwa kuwa ripoti yake ilionekana kutetea Serikali pekee na jeshi la polisi na hivyo wabunge wa chama pinzani wakaendelea na msimamo huku wakisema hivyo nikudidimiza haki za kila raia kwa kuruhusu machafuko yaendelee kufuatia kauli kama hizo,huku vyombo vya habari vikiwa vimeonyesha namna ambavyo Jeshi la Polisi lilitumia nguvu kubwa bila sababu  kudhibiti maandano hayo ya CUF  Juzi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment