Mabadiliko ya Baraza la mawaziri
alilofanya Rais Jakaya Kikwete viongozi
mbalimbali wa vyama vya siasa na Dini pamoja na
wananchi wa kawaida wametoa maoni yao huku wengine wakipongeza huku mwenyekiti wa taifa wa chama cha Demokrasia na
maendeleo chadema mhe Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa ukawa akisema hakuna jambo jipya kwa sababu bado sura ni zile zile.
Mh.Mbowe amesema hakuna jambo
jipya katika baraza hilo kutokana na ukweli
kuwa watu ni wale wale ila amebadilishwa wizara na hivyo ni sawa na kwamba hakijafanyika chochote.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
taifa wa jumuiya ya wazazi chama cha mapinduzi CCM Mh. Abdalah Bulembo amesema mabadiliko aliyoyafanya Rais ni yenye tija
na kuongeza kuwa kitendo cha Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu ni
ishara ya kukubali matokeo ili kukinusuru chama cha mapinduzi.
Naye Sheikh Rajabu Katimba ambaye
ni msemaji wa jumuiya ya taasisi za
kislamu amesema kujiuzulu Prof
muhongo na kuteua baraza lingine siyo Dawa peke bali waliokula fedha za umma wawajibishwe.
Kwa upande wawananchi Bi.Mary Massawe na Bw .Peter Karia wamewataka viongozi waliobaki
madarakani kutambua kuwa wamepewa jukumu kubwa na wajifunze kutoka kwa wenzao
kwani taifa linawategemea na siyo kufanya mambo kama vile nchi haina.
0 comments:
Post a Comment