TANZANIA bado inakabiliwa na tatizo la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ambapo kwa takwimu za hivi karibuni watoto waliotambuliwa kuishi katika mazingira hayo ni 897,913, wanaume wakiwa asilimia 53 na wasichana asilimia 47.
Hayo yalibainika jana wakati wa kongamano la siku tatu la kitaifa la watoto walio katika mazingira hatarishi lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal akizungumza katika ufunguzi wa kongamano hilo alisema limekuja wakati muafaka wakati taifa bado linakabiliwa na tatizo la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
“Hali ya mazingira ya watoto hapa nchini bado hairidhishi, watoto wengi wanaishi katika mazingira hatarishi wakiwa katika umri mdogo. Watoto hawa wako katika hatari ya kupata makuzi mabaya, athari za kimwili, kiakili na kisaikolojia,”alisema.
Kwa mujibu wa Dk Bilal, watoto 897,913 wanaishi katika mazingira hatarishi, watoto milioni 2.5 wakiwa yatima kutokana na ugonjwa wa Ukimwi, watoto wa kike watatu kati ya 10 wakifanyiwa ukatili wa kingono na watoto wa kiume saba kati ya 10 wakifanyiwa ukatili wa kingono na kwamba robo ya watoto hufanyiwa ukatili wa kimwili wakiwa chini ya miaka 18.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto(UNICEF), Dk Jama Gulaid alisema Tanzania inaweza kuwa nchi nzuri ya kuishi watoto kama ilivyo nchi ya Mauritius iwapo mianya inayotoa nafasi ya watoto kuishi maisha yasiyo salama inazibwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment