Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana BAN KI-MOON amepongeza makubaliano ya hivi karibuni ya kusitisha mapigano kati ya pande mbili zinazohasimiana Sudan Kusini.Hata hivyo Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameonesha kusikitishwa kwake na pande hizo mbili kutokubaliana namna ya mgawanyo wa madaraka.Msemaji wa Bwana BAN amewaambia Waandishi wa Habari kuwa hakutapatikana amani Sudan Kusini iwapo Rais SALVA KIIR na kiongozi wa waasi, Bwana RIEK MACHAR hawataweka mbele maslahi ya raia.Msemaji huyo Bwana STEPHANE DUJARRIC amesema Umoja wa Mataifa hauna taarifa za mapigano mapya tangu pande hizo zinazopingana Sudan Kusini kutiliana saini juzi.Serikali ya Sudan Kusini na waasi zimekubaliana kukamilisha makubaliano ya kukomesha mgogoro wa nchi hiyo uliodumu kwa mwaka mmoja sasa itakapofika tarehe tano mwezi ujao.
Home
News
BAN KI-MOON apongeza makubaliano ya mahasimu wa wili wa Sudan Kusin kukubaliana kusitisha mapigano,licha ya kutokukubaliana katika mgawanyo wa madaraka
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment