Image
Image

Hollande kukutana na vyombo vya habari


François Hollande anatazamiwa Alhamisi wiki hii kufanya mkutano wake wa tano na vyombo vya habari kila baada ya miezi sita tangu achaguliwe kuwa rais.
Mkutano huo unatazamiwa kufanyika, baada ya Ufaransa kukumbwa na mfululizo wa mashambulizi mwezi uliyopita.

Rais wa Ufaransa, atajibu maswali ya waandishi wa habari kwenye Ikulu ya Champs Elysée saa tano, saa za Paris.

Rais Hollande amekua akifanya mkutano na waandishi wa habari kila baada ya miezi sita, lakini mkutano huu, utagubikwa na hali inayojiri Ufaransa, baada ya mashambulizi yaliyoikumba nchi hii tangu Januari 7 hadi 9 mwaka 2015.

Shambulio dhidi ya jarida la vibonzo la Charlie Hebdo lililogharimu maisha ya watu wakiwemo wachoraji maarufu wa jarida hilo pamoja na askari polisi, mtazamo wa Januari 11, ambapo François Hollande anatarajia kutumia ili kufufua miaka yake mitano.

Washirika wake wa karibu wanajua kwamba rais Hollande anajaribu kurejesha imani kwa raia. Kwa mara ya kwanza tangu miaka kadha iliyopita, François Hollande amepoteza imani kwa raia wake.

Watu wengi wamekua wakijiuliza François Hollande ataelekea wapi? Kutakuwa na matangazo katika mkutano wa wanahabari juu ya elimu, dhamira ( ya vijana ikiwa ni pamoja na huduma ya kiraia), maadili ya kitaifa au ubaguzi kufuatia maeneo mbalimbali ya nchi, kulingana na istilahi inayotumiwa na Ikulu ya Elysee, ikimaanisha "ubaguzi wa rangi" ambao Waziri mkuu, Manuel Valls, alilani hivi karibuni.

Nasubiri " Mpango wa Kijamhuri" ambao utapelekea kujenga upya vitongoji ambavyo vimekua katika mazingira magumu, lakini pia kuhakikisha na kutoa ahadi za kazi kwa kina baada ya muda, amesema rais Hollande. Hayo ndio Wabunge wanatarajia kutoka katika maswali na majibu.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment