RAIS Jakaya Kikwete ameamua kufumua safu yake ya Wakuu wa Wilaya na wengine akiwaachia kazi ambapo mabadiliko hayo yametafsiriwa na wachambuzi wa siasa nchini kama sehemu ya mabadiliko ya mwisho kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Wakizungumzia mabadiliko hayo wachambuzi hao wa siasa mbalimbali nchini walisema jana kuwa mabadiliko hayo huenda Rais Kikwete ameamua kuvunja mtandao wa urais katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi huku wengine wakidai kuwa wakuu wa wilaya walioachwa huenda imetokana na ujenzi wa maabara ambapo rais alikuwa mkali na alishatoa tahadhari mapema.
Akitangaza mabadiliko hayo jana mkoani hapa, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema Rais Kikwete amefanya uteuzi wa wakuu wa wilaya wapya 27 na mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya wakuu wa wilaya wa mwanzo kwa lengo la kuboresha utendaji Serikalini.
Pinda alisema, mabadiliko hayo yamezingatia kuwepo kwa nafasi 27 zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali. Alizitaja sababu hizo kuwa ni kufariki kwa wakuu wa wilaya watatu, wakuu wa wilaya watano kupandishwa vyeo kuwa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya saba kupangiwa majukumu mengine huku wakuu wilaya 12 wakitenguliwa uteuzi wao.
Alisema katika mchakato huo,wakuu wa wilaya 64 wamebadilishwa vituo vya kazi na wakuu wa wilaya 42 wameendelea katika vituo vyao vya kazi vya awali.
Ma-DC wapya
Pinda aliwataja wakuu wa wilaya wapya kuwa ni pamoja na Mariam Mtima (Ruangwa), Dk. Jasmine Tiisike (Mpwapwa), Pololeti Mgema (Nachingwea), Fadhili Nkurlu (Misenyi), Felix Lyaniva (Rorya), Fredrick Mwakalebela (Wanging’ombe) na Zainabu Mbussi (Rungwe).
Wengine ni Francis Mwonga(Bahi), Kiming’ombe Nzoka (Kiteto), Husna Msangi (Handeni), Emmanuel Uhaula (Tandahimba), Mboni Mhita (Mufindi),Hashim Mgandilwa (Ngorongoro), Mariam Juma (Lushoto), Thea Ntara (Kyela), Ahmad Nammohe (Mbozi) na Shaaban Kisu ( Kondoa).
Majina mengine ni Zelothe Steven (Musoma), Pili Moshi (Kwimba), Mahmoud Kambona (Simanjiro) ,Glorius Luoga (Tarime),Zainabu Telack (Sengerema),Benard Nduta (Masasi),Zuhura Ally (Uyui) ,Paul Makonda (Kinondoni), Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na Maftah Mohamed (Serengeti).
Waliotemwa
Pinda aliwataja waliotenguliwa uteuzi wao kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiumri, kiafya kuwa ni pamoja na James Millya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Longido, Elias Lali aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Alfred Msovella aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kongwa, Danny Makanga aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Kasulu, Fatma Kimario aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.
Wengine waliotenguliwa ni Elibariki Kingu aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Igunga, Dk.Leticia Warioba aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Iringa, Evaristi Kalalu aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Mufindi, Abiud Saidea aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Momba, Martha Umbulla aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kiteto, Khalid Mandia aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Babati na Elias Goroi.
Wanaosubiri majukumu mengine
Pinda aliwataja wakuu wa wilaya ambao uteuzi wao umetenguliwa na kupangiwa majukumu mengine ni wakuu wa wilaya saba ambao ni Brigedia Generali Cosmas Kayombo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Kanali Ngemela Elson Lubinga aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Mlele na Juma Madaha aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Ludewa.
Pia wamo, Mercy Silla aliyekuwa mkuu wa wilaya Mkuranga , Ahmed Kipozi aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mrisho Gambo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Korogwe na Elinas Pallangyo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Rombo.
Waliobadilishwa vituo
Pinda alisema wakuu wa wilaya waliobadilishwa vituo ni Nyerembe Munasa (Arumeru-Mbeya), Jordan Rugimbana Kinondoni-Morogoro) Fatma Ally(Chamwino-Mtwara), Lephy Gembe (Dodoma Mjini-Kilombero), Christopher Kangoye(Mpwapwa-Arusha).
Wengine ni Omar Kwaang’ (Kondoa-Karatu), FrancisMtinga(Chemba-Muleba) Elizabeth Mkwasa(Bahi-Dodoma), Agnes Hokororo (Mb) (Ruangwa-Namtumbo), Regina Chonjo (Nachingwea-Pangani), Husna Mwilima (Mbogwe-Arumeru), Gerald Guninita (Kilolo- Kasulu)
Pia wamo Zipporah Pangani(Bukoba-Igunga), Kanali Issa Njiku (Missenyi-Mlele), Richard Mbeho(Biharamulo-Momba), Lembris Kipuyo (Muleba-Rombo), Ramadhani Maneno (Kigoma-Chemba), Venance Mwamoto(Kibondo-Kaliua),Gishuli Charles(Buhigwe-Ikungi),
Novatus Makunga (Hai-Moshi), Anatory Choya (Mbulu-Ludewa).
Wengine ni Christine Mndeme(Hanang’-Ulanga), Jackson Musome (Musoma-Bukoba), John Benedict Henjewele (Tarime-Kilosa), Dk. Norman Sigalla(Mbeya-Songea), Dk. Michael Kadeghe (Mbozi-Mbulu), Crispin Meela (Rungwe-Babati), Magreth Malenga (Kyela-Nyasa) na Said Amanzi (Morogoro-Singida).
Pinda aliwataja wengine ni Antony Mtaka (Mvomero-Hai), Elias Tarimo (Kilosa-Biharamulo) Francis Miti (Ulanga-Hanang’), Hassan Masala (Kilombero-Kibondo), Angelina Mabula(Butiama-Iringa), Farida Mgomi (Masasi-Chamwino), Wilman Ndile (Mtwara-Kalambo), Ponsian Nyami (Tandahimba-Bariadi), Mariam Lugaila (Misungwi -Mbogwe) na Mary Onesmo(Ukerewe-Buhigwe).
Pia Karen Yunus (Sengerema-Magu), Josephine Matiro (Makete-Shinyanga), Joseph Mkirikiti (Songea-Ukerewe), Abdula S Lutavi (Namtumbo-Tanga), Ernest Kahindi (Nyasa-Longido), Anna Rose Nyamubi(Shinyanga-Butiama), Rosemary Kirigini (Mb) (Meatu-Maswa),
Abdallah Kihato (Maswa-Mkuranga).
Wengine ni Erasto Sima (Bariadi-Meatu), Queen Mulozi(Singida -Urambo), Yahya Nawanda(Iramba-Lindi), Manju Msambya (Ikungi-Ilemela), Saveli Maketta(Kaliua-Kigoma), Bituni Msangi(Nzega-Kongwa), Lucy Mayenga(Uyui-Iramba), Majid Mwanga(Lushoto-Bagamoyo), Muhingo Rweyemamu (Handeni -Makete), Hafsa Mtasiwa (Pangani-Korogwe).
Pinda aliwataja wengine Dk. Nasoro Hamidi (Lindi-Mafia), Festo Kiswaga (Nanyumbu-Mvomero), Sauda Mtondoo (Mafia-Nanyumbu), Seleman Mzee Seleman (Kwimba-Kilolo),Esterina Kilasi (Wanging’ombe-Muheza), Subira Mgalu (Muheza -Kisarawe) na Jacqueline Liana (Magu -Nzega).
Waliobaki vituo vyao kazi
Wakuu wa Wilaya wafuatao wanaendelea kubaki katika vituo vyao vya sasa ni Jowika Kasunga(Monduli), Raymond Mushi (Ilala-), Sophia Mjema(Temeke), Amani Mwenegoha (Bukombe), Ibrahim Marwa (Nyang’wale), na Rodrick Mpogolo (Chato), na Manzie Mangochie (Geita).
Pia Darry Rwegasira (Karagwe), Luteni Kanali Benedict Kitenga(Kyerwa), Constantine Kanyasu(Ngara), Paza Mwamulima(Mpanda), Peter Kiroya (Kakonko), Hadija Nyembo(Uvinza), Dk. Charles Mlingwa (Siha), Shaibu Ndemanga (Mwanga), Herman Kapufi (Same), Ephraim Mbaga(Liwale), Abdallah Ulega (Kilwa).
Pia Joshua Mirumbe (Bunda), Deodatus Kinawiro (Chunya), Rosemary Senyamule (Ileje), Gulamhusein Shaban (Mbarali), Christopher Magala (Newala), Baraka Konisaga (Nyamagana), Sarah Dumba (Njombe), Hanifa Karamagi (Gairo), Halima Kihemba (Kibaha), Nurdin Babu(Rufiji), Mathew Sedoyeka(Sumbawanga).
Wengine ni Idd Kimanta(Nkasi), Chande Nalicho (Tunduru), Senyi Ngaga (Mbinga), Wilson Nkambaku (Kishapu), Benson Mpesya (Kahama), Paul Mzindakaya (Busega),Georgina Bundala (Itilima), Fatuma Toufiq(Manyoni), Luteni Edward Ole Lenga (Mkalama), Hanifa Selengu(Sikonge), Suleman Kumchaya(Tabora), Mboni Mgaza (Mkinga), Seleman Liwowa (Kilindi).
Waliofariki dunia
Kwa mujibu wa Pinda wakuu wa wilaya waliofariki kuwa ni Kaptein Yamungu aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Serengeti, Anna Magoha aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Urambo na Moshi Chang’a aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kalambo.
Waziri Mkuu Pinda amewataka wakuu wa wilaya waliobadilishwa vituo kuanza kazi mara moja huku akisema wapya wanasubiri kupatiwa mafunzo ili kuboresha uwajibikaji wao.
Akizungumzia uteuzi huo, Paul Makonda ambaye anakuwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam alisema, kwanza anamshukuru Mungu kwa kuwa kila hatua ya uongozi hupangwa na Mungu.”Asante Mungu”.
Pia alisema anamshukuru Rais Kikwete kwa uamuzi wake wa kumteua katika nafasi hiyo ili aweze kushiriki katika ujenzi wa Taifa, huku akitumia nafasi hiyo kuomba ushirikiano kutoka kwa anaokwenda kuwatumia.
Home
News
JK apangua mtandao wa urais apangua Ma-DC wake, aamua kuwatema 12 *Ateua wengine wapya 27, wamo wanaosubiri majukumu
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment