Mbunge
wa kilolo Prof. Peter Msola ameshindwa kulipatia suluhu
swala hilo na kuondoka eneo la tukio huku polisi wakibaki na maiti kwenye
gari.
Tukio hilo lilitokea juzi mkoani Iringa ambako mtu mmoja alifariki
wakati wananchi walipopambana na polisi na baadaye kufunga barabara kwa
saa tano, limeingia katika orodha ndefu ya matukio yanayozidi kuongezeka
kila kona ya mapambano baina ya raia na askari wa Jeshi la Polisi.
Katika tukio la juzi, wananchi wa Ilula
walimtuhumu polisi kumuua mwanamke kwa kosa la kuuza pombe muda wa kazi
na hivyo kupanda ghadhabu na kuvamia kituo cha polisi ambako walichoma
magari matano madogo na basi moja na baadaye kwenda kufunga Barabara ya
Dar es Salaam- Mbeya kwa muda wa saa tano hadi Jeshi la Polisi
lilipoongeza askari wake kutuliza ghasia hizo.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoani Iringa,
Pudensiana Protas aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa watu 18
wamekamatwa wakihusishwa na vurugu hizo, lakini akakataa kuzungumzia
mwanamke aliyekufa akisema atafanya hivyo baada ya kupokea taarifa ya
daktari.
Tukio hilo ni moja tu kati ya mengi ambayo
yamekuwa yakitokea katika miezi ya karibuni yakihusisha wanavijiji,
walimu, wakulima, wasomi, madaktari, wanafunzi wa sekondari na makundi
ya vijana ambao katika kushinikiza wanasikilizwa au kulinda haki zao,
wamejikuta wakifanya vurugu zinazohusisha mapambano dhidi ya askari wa
Jeshi la Polisi, uharibifu wa vyombo vya usafiri, kufunga barabara na
maandamano ambayo hukatishwa kwa virungu, mabomu ya machozi na wakati
mwingine silaha
0 comments:
Post a Comment