Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Shamariwa 'A' Kata ya Igoma Jijini Mwanza, Bwana JULIAS MAKOYE amekutwa amejinyonga juu ya mti uliopo jirani na nyumba yake usiku wa kuamkia jana.
Mke wa marehemu MAKOYE, Bibi IVONA POLIKALAPO amesema mwili wa mume wake ulikutwa ukining'inia juu ya mti huku mbwa wakibweka .
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Bwana JAPHET LUSINGU, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, ingawa hakuwa tayari kueleza sababu za kifo hicho.
Marehemu MAKOYE alichaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Kishiri ' A ' kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Desemba 14 mwaka jana kwa awamu ya pili.
Habari zaidi zinasema juzi majira ya saa 10 jioni Bibi IVONA alimsikia mumewe akizungumza na mtu kwenye simu yake ya mkononi na aliyekuwa akizungumzia naye kumsisitiza kuwa anahitaji mzigo wake wote kutokana na kukaa muda mrefu.
Amesema hata hivyo mtu aliyekuwa akizungumza na mume wake hakumfahamu.
Picha kwa hisani ya Maktaba yetu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment