Mbarali.
Wapo wastaafu wengi wa Serikali ambao
wanafuatilia kwa karibu nyenendo za siasa nchini, mmoja wapo ni Kanali
Mstaafu Edmund Mjengwa (68) ambaye amekitahadharisha chama cha CCM
kwamba kijiandae kwa Serikali ya mseto.
“Na endapo Rais atatoka CCM na wabunge wengi ndani
ya Bunge wakawa ni wa upinzani, basi lazima Rais huyo akubali kufanya
kazi na upinzani.
“Itabidi akubali kuunda Serikali ya mseto, japo
sitarajii kufika huko. CCM ni imara, lakini tuwe na fikra hizo pia kwa
nia nzuri ya kuiweka nchi katika amani,” ni kauli ya Kanali Mjengwa
ambaye pia ni mkuu wa wilaya mstaafu.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili nyumbani
kwake Mbarali, Kanali Mjengwa alisema licha ya upinzani kuwepo na
kujipambanua kwa wananchi, lakini bado siyo tishio kwa CCM na itaendelea
kushika dola tu kwani inaaminika na Watanzania wengi.
“Upinzani kuingia Ikulu bado sana, ila kwenye
nafasi ya ubunge na udiwani ndiko kutakuwa na changamoto kubwa. Kuna
uwezekano mkubwa wa wabunge wengi wakatoka upinzani lakini siyo Rais.
“Lakini niseme tu kwamba pamoja na CCM kuendelea
kuaminiwa na wananchi wengi, isibwete wala kupuuza upinzani. Hawa jamaa
wanazidi kujitanua kweli kweli, hivyo wanaweza kuiyumbisha,” alisema
Kanali Mjengwa.
Kanali Mjengwa alisema CCM bado inaaminiwa na
Watanzania wengi, lakini tatizo linalomkera na mabalo kwa maoni yake
linaharibu adabu na sifa ya CCM ni kitendo cha wana-CCM kuchafuana
majukwaani.
Alisema CCM imetoka mbali na inatakiwa kuongoza
kwa vitendo na siyo kupiga kelele za kuchafuana majukwaani kama ambavyo
ilivyo hivi sasa.
Kwa mujibu wa Kanali Mjengwa anachukia kuona
mwana-CCM anatumia jukwaa kumchafua mwenzake kisa tu wote wametangaza
nia ya kugombea nafasi fulani ya uongozi.
“Kama unona mwana CCM fulani amekwenda ndivyo
sivyo kuna taratibu za vikao ndani ya chama, wakazungumzie na kumaliza
tofauti hizo ndani ya Chama ili kulinda heshima ya Chama na si
vinginevyo.
“Na kitendo hicho ndicho kinachowapa nguvu
wapinzani kwa kusemea na kutunanga kwa Wananchi hatimaye CCM inaonekana
kutokuwa na watu makini,” alisema.
Kanali Mjengwa alisema katika kuelekea uchaguzi
mkuu hali ya kisiasa inazidi kupamba moto na kila chama kinazidi
kujipambanua kivyake kwa wananchi kikitaka kuungwa mkono.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment