|
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Hassan Kimanta
akitoa salam za pongezi kwa Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Msaada wa watu
wa Marekani katika kusaidia ujenzi wa barabara za lami Mkoani Rukwa. |
|
Baadhi ya
viongozi katika meza kuu wakifuatilia jambo katika mkutano huo wa hadhara.
|
|
Waziri
wa Wizara ya Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiagwa
kwa shangwe na wananchi wa Mjini Sumbawanga mara baada ya hotuba yake nzito
kuhusu ujenzi wa barabara iliyowafurahisha wengi katika mkutano wa
hadhara uliofanyika katika viwanja vya Nelson Mandela.
|
|
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akiteta jambo na
Waziri wa Wizara ya Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli muda mfupi kabla ya
kumaliza ziara yake Mkoani Rukwa na kuendelea na ziara yake Mkoani
Katavi leo tarehe 03/02/2015.
| |
|
|
|
|
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya katikati
akizungumza leo tarehe 03/02/2015 kwenye ziara ya Waziri wa Wizara ya Ujenzi
Mhe. Dkt John Pombe Magufuli wa pili kushoto ambapo aliishukuru Wizara ya
Ujenzi kwa juhudi ilizofanya katika ujenzi unaoendelea wa barabara za lami
Mkoani Rukwa. Pamoja na hayo ameiomba Serikali kupitia Wizara hiyo kusaidia pia
katika ujenzi wa barabara muhim za Wampembe iliyopo Wilaya ya Nkasi,
barabara ya bondeni kwa ajili ya kuunganisha ukanda wa bonde la Ziwa Rukwa
unaoongoza kwa uzalishaji wa mpunga na Mikoa ya Katavi
na Mbeya, barabara ya Kasesha kwa ajili ya kuunganisha Mkoa wa Rukwa na Zambia
na barabara ya kuelekea Kalambo Falls yalipo maporomoko ya Mto Kalambo ambayo
ni ya pili kwa urefu barani Afrika.
|
Barabara ya Tunduma-Ikana-Laela hadi Sumbawanga
ikiwa imekamilika kwa asilimia mia moja (100%), barabara hii ambayo ni kiungo
muhimu cha Mikoa ya Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma na Tabora imejegwa kwa
ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Msaada kutoka kwa watu wa Marekani.
Waziri wa Wizara ya Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi
wa Mjini Sumbawanga tarehe 02/02/2015 katika viwanja vya Nelson Mandela akiwa
ziarani Mkoani Rukwa kukagua ujenzi unaoendelea wa barabara za lami za
Tunduma-Ikana-Laela-Sumbawanga, Sumbawanga-Matai-Kasanga na Sumbawanga-Kanazi-Kizi-Kibaoni
hadi Mpanda.
Katika hotuba yake hiyo aliwaahidi wananchi wa Mkoa wa Rukwa juu ya dhamira ya
dhati ya Serikali iliyopo madarakani kukamilisha ujenzi wa barabara za lami
kuunganisha Mikoa ya Mbeya-Katavi-Kigoma na Tabora. Alisema hayo yatafanikiwa
iwapo wananchi watatoa ridhaa kwa Serikali iliyopo madarakani kuendelea
kuingoza nchi kwa miaka mingine mitano ijayo iweze kufikia malengo
iliyojiwekea.
Mradi wa barabara ya Tunduma-Sumbawanga umekamilika kwa asilimia mia moja na
Mhe. Waziri ameahidi Wizara yake kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya barabara
zilizobakia zikiwemo barabara za Manispaa ya Sumbwanga na zile za Wilaya ya
Nkasi. Kwa ujumla fedha alizoahidi kusaidia eneo la Manispa na Wilaya ya Nkasi
ni zaidi ya Tsh bilioni nne.
Kwa mujibu wa Mhe. Magufuli miradi yote mikubwa ya ujenzi wa barabara Mkoani
Rukwa inagharimu fedha za kitanzania zaidi ya shilingi bilioni mia nane (800),
ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Serikali iliyopo
madarakani (CCM)
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment