Mvua ya mawe iliyokuwa imeambatana na upepo mkali
imesababisha maafa ambapo watu 35 wamefariki huku 55 wakijeruhiwa kutokana na
kuangukiwa na nyumba zao kutokana na mvua hiyo kuambatana na upepo mkali
Wilayani kahama mkoani shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na yupo katika eneo la tukio kusimamia zoezi la kuokoa majeruhi
na kufukua miili ya marehemu.
Hata hivyo kwa upande mwingine Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Justus Kamugisha akizungumza kwa njia ya simu amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo ambapo amesema kuwa watu waliofariki dunia kutokana na mafuriko hayo wameangukiwa na nyumba na miti hadi kupoteza maisha ambapo amesema hadi sasa wamethibitisha watu 38 wamepoteza maisha huku 55 wakiwa majeruhi.

0 comments:
Post a Comment