MECHI ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya wenyeji, Yanga SC
dhidi ya timu ya FC Platinum ya Zimbambwe iliyofanyika mwishoni mwa wiki
katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam iliingiza mil 91,660,000
kutokana na watazamaji 14,563 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.
Mgawanyo
wa mapato katika mchezo huo ni, VAT 18% sh. 13,982,033, Gharama ya
tiketi sh. 12,380,000, Uwanja 15% sh. 9,794,694.92, Gharama za mchezo
15% sh. 9,794,694.92, TFF 5% sh. 3,264,898.31, CAF 5% sh. 3,264,898.31
na Young Africans 60% sh.39.178,779.66.
Katika mchezo huo wa
kwanza wa Raundi ya Kwanza ya michuano hiyo, Yanga SC ilianza kwa
ushindi wa 5-1 nyumbani dhidi ya Platinum FC na sasa itakwenda kupigania
hata sare ugenini wiki ijayo ili kusonga mbele.
Salum Telela akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao la kwanza katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Platinum Jumapili
Home
MICHEZO
MECHI ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya wenyeji, Yanga SC dhidi ya timu ya FC Platinum ya Zimbambwe iliingiza mil 91,660,000
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment