Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshugulikia Elimu, KASSIM MAJALIWA
Serikali imesema inatambua mchango wa sekta binafsi unaochangiwa katika
elimu wenye lengo la kuboresha elimu nchini kwa kuweka miundombinu
inayofaa.
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa majengo ya Shule ya Msingi ya
MAKTABA iliyopo UPANGA Jijini DSM Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshugulikia Elimu KASSIM
MAJALIWA amesema michango kama hiyo inaunga mkono mikakati ya serikali
ya maendeleo ya elimu ya msingi na sekondari pamoja na Mpango wa Matokeo
Makubwa Sasa -BRN
Maktaba iliyopo imetolewa na Jumuiya ya Dini ya BAPS Charities
ambapo mwenyekiti wa Jumuiya hiyo SUBHASH PATEL amesema jumuiya yao
inaelewa umuhimu wa elimu hivyo itaendelea kushirikiana na serikali
katika sekta ya elimu na kuwaomba wadau wengine wa elimu kujitokeza
katika kuchangia kuboresha elimu nchini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment