Serikali
imetakiwa kuweka sheria kali za kuwadhibiti wawekezaji ambao wanakiuka miiko ya
uwekezaji kwa kubadili miradi katika eneo husika tofauti na ule waliomba
kuufanya.
Mbunge wa
Viti maalum kupitia chama cha mapinduzi Ester Bulaya ametoa ushauri huo bungeni
mjini Dodoma ambapo Naibu Waziri ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na
Serikali za mitaa Khasim Majaliwa ameziagiza halmashauri zote nchini
kutoa taarifa Serikali kuu kuhusiana na wawekezaji waliokiuka miiiko ya uwekezaji
kwa kubadili miradi pasipo taarifa.
0 comments:
Post a Comment