Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani
mkoa wa Iringa Salim Asas (kulia) akimtazama mmoja
kati ya majeruhi 22 waliolazwa katika Hospitali ya wilaya
ya Mufindi mkoani Iringa ambao walipata ajali mbaya baada
ya basi la majinja lenye namba za usajili T348 CDE kugongana na lori
na kufunikwa na kontena lake jana eneo la Changalawe nje kidogo
ya mji wa Mafinga ,katika ajali hiyo watu 42
walifariki dunia.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza
wa pili kulia akiwa na viongozi mbali mbali wa
tatu ni kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi ,
akifuatiwa na mwenyekiti wakamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa
Salim Asas na mkuu wa wilaya ya Mufindi Mboni Mhita jana walipofika
eneo la ajali iliyoua 42 na kujeruhi 22 .
Basi la Majinja likiwa limefunikwa na kontena baada ya ajali iliyohusisha basi hilo na Lori baada ya kugongana yso kwa uso Mafinga mkoani Iringa.Eneo hili ndilo lililo sababisha ajali licha ya Magari hayo kuwa mwendo kasi lakini Mashimo haya yalielezwa kuchangia ajali hiyo.
Baadhi ya Majeruhi wa ajali hiyo wakiwa wamelala kitandani katika hospitali ya Mufindi iringa kwaajili ya kupatiwa matibabu kufuatia majeraha wakiyoyapata kufuatia ajali hiyo.
Hili ni Ambulance ilipokuwa katika eneo latukio ikiwa inabeba miili ya watu waliopoteza maisha.
Badhi ya watu katika eneo hilo la tukio wakiwa wanaangalia hali ilivyokuwa huku wakiwa na mshangao na kubaki na sinto amini kwa ajali iliyotokea na kugharimu maisha ya wapendwa wetu 42 Mafinga Mkoani Iringa.
Watu 42 wamepoteza maisha na wengine 23 kujeruhiwa baada ya lori la mizigo kugongana na basi na kontena lililokuwa limebebwa kuangukia gari hilo la abiria, katika ajali ya aina yake iliyotokea eneo la Mafinga Changalawe mkoani Iringa.
Watu 37 waliokuwa kwenye basi hilo la kampuni ya
Majinjah Express lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam,
walifariki papo hapo na wengine watano kufariki wakiwa Hospitali ya
Mafinga. Dereva wa basi na wa lori hilo la kampuni ya Cipex, pia
wamefariki.
Shuhuda mmoja wa ajali hiyo, Nyasio Pascal,
aliyekuwa akiendesha basi la Saibaba, alisema aliliona lori hilo
likijaribu kukwepa mashimo kwenye barabara hiyo ambayo ni nyembamba, na
mara likaanza kuyumba kulia na kushoto baada ya kukanyaga shimo na ndipo
lilipolifuata basi na kugongana nalo.
Alisema kontena lililokuwa limebebwa na lori hilo,
liliangukia juu ya basi na kulikandamiza, jambo ambalo lilisababisha
vifo vya watu wengi na pia kuzuia watu waliokuwa karibu na ajali kuokoa
watu waliojeruhiwa hadi tingatinga lilipowasili. Hata hivyo, alisema
mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja, alinusurika kwenye ajali hiyo
bila ya kudhurika.
Miili ya waliokufa imehifadhiwa kwenye Hospitali
ya Mafinga, ambayo ina chumba cha kuhifadhia miili ya watu saba tu, na
mingine imepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Iringa.
“Hii ni ajali mbaya ambayo haijawahi kutokea
mkoani hapa,” alisema mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza aliyefika
eneo hilo la ajali.
Wanaume saba na wanawake 35 wamepoteza maisha kwenye ajali hiyo, iliyochukua maisha ya watoto watatu.
Katika eneo hilo ambako ajali hiyo imetokea hali
ilikuwa mbaya kutokana na kontena la lori hilo kulalia basi na
kukandamiza miili ya abiria, jambo ambalo lilisababisha ugumu katika
kuokoa abiria waliokuwemo ndani ya basi.
Polisi wakishirikiana na watoa huduma ya afya
kutoka Mufindi walifika kusaidia katika kutoa huduma ili kuokoa wale
ambao walikuwa wamejeruhiwa na kuhitaji matibabu ya haraka.
Tingatinga lilifika na kusaidia kulinyanyua
kontena na hivyo kurahisisha kazi ya kutoa miili ya wale waliokuwa
wamebanwa na miili ya waliokufa pia.
Majeruhi wazungumza
Kevin Humprey, aliyekuwa amekaa viti vya nyuma
kwenye basi hilo, alisema alisikia kishindo kimetokea na kuona kontena
limelalia sehemu kubwa ya basi.



0 comments:
Post a Comment