Image
Image

Tuongeze uwekezaji viwanda vinaweza

RIPOTI ya karibuni zaidi ya jarida la The Economist maarufu kwa jina la Pocket World in Figures, imeonyesha kwamba Tanzania hivi sasa ni nchi ya 14 duniani kwa ukuaji wa uzalishaji viwandani.
Taarifa hizi zimekuja katika kipindi ambacho Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndullu, ametangaza kwamba hivi sasa sekta ya uzalishaji inaliingizia Taifa fedha nyingi za kigeni kuliko hata dhahabu ambayo imekuwa kinara kwa takribani muongo mmoja uliopita.
Takwimu hizo za The Economist zimechukuliwa katika kipindi cha kati ya mwaka 2011 hadi 2013 na Tanzania inazidiwa na nchi sita tu za Afrika katika orodha hiyo ya nchi 20 bora.
Habari hizi ni njema kwa sababu katika miaka ya karibuni, uzalishaji katika viwanda ulishuka sana na inaonekana Taifa lilijilegeza kwa kutegemea mapato ya dhahabu pekee.
Kushuka kwa bei ya dhahabu kunatakiwa kufumbua macho ya serikali na sekta binafis kutazama fursa mbalimbali zilizopo katika eneo la viwanda.
Ni wazi kwamba kama uzalishaji huu wa viwandani utapewa kila aina ya msaada unaohitajika, Tanzania inaweza kuingiza fedha nyingi zaidi za kigeni kuliko dola bilioni 1.4 zilizopatikana katika mwaka uliopita.
Nchi hii bado inahitaji viwanda zaidi vya saruji, vya kutengeneza nyuzi, unga wa ngano na sembe na usindikaji ili kuweza kuingiza fedha hizo za kigeni. Viwanda hivi vikiongezeka, wakulima wa mazao yanayotoa nyuzi kama vile pamba nao watapata masoko ya bidhaa zao.
Kubwa zaidi, viwanda hivi vitakuwa chachu kubwa ya kupambana na tatizo la ajira ambalo limeanza kuwa kubwa na linalohatarisha amani na ustawi wa Taifa letu.
Wakati tukifanya kila jitihada na uchumi wa gesi na mafuta unatarajiwa kuleta mabadiliko katika kipindi cha miaka kumi ijayo, ni vema tukaelewa kuwa uhakika zaidi upo kwenye kilimo na viwanda kuliko madini au nishati nyingine ambazo huwa zinamalizika.
Wakati umefika sasa wa serikali na sekta binafsi kukaa na kutafakari ni wapi na lini viwanda vingine zaidi vifunguliwe ambavyo vitaongeza mapato ya Taifa, kusaidia wakulima na pia kukuza ajira.
Wakati ni huu. - See more at: http://www.raiamwema.co.tz/tuongeze-uwekezaji-viwanda-vinaweza#sthash.13Y1hkiw.dpuf

Wakati ni huu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment