Wakaazi wa mkoa wa MANYARA, wametakiwa kulisaidia jeshi la polisi mkoani
humo kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na
watoto vilivyokithiri mkoani humo ili kukomesha vitendo hivyo
vinavyokwenda kinyume na haki za binadamu.
Wito huo umetolewa mjini BABATI mkoani humo na Mkuu wa Dawati la
Jinsia na Watoto, Naibu Kamishina wa Polisi -DCP ADOLFINA CHIALO, wakati
akifungua mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo maafisa na wakuu wa
dawati la Jinsia na watoto kutoka jeshi la polisi mkoani Manyara
Mafunzo hayo yanafanyika huku Takwimu zilizotolewa miaka miwili
iliyopita na Wizara ya Afya na Usatwi wa Jamii zikibainisha kuwa mkoa wa
Manyara, umekuwa kinara wa matukio ya ukeketaji ambapo inadadiriwa kuwa
asilimia 15 ya wanawake wa mkoa huo wamekeketwa huku kiwango cha
ukatili wa namna hiyo kikifikia asilimia 71, na kufuatiwa na mikoa ya
Dodoma, ARUSHA, SINGIDA, MOROGORO na TANGA ambavyo ukatili umefikia kati
ya asilimia 20 hadi 64.
Kutokana na changamoto hizo Mtandao wa Kijinsia hapa nchini-TGNP kwa
kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulika na masuala ya
idadi ya watu duniani, UNFPA na Shirika la GTI, wamefadhili na kuendesha
mafunzo ya namna ya kushughulikia makosa ya unyanyasaji na ukatili huo
wa Kijinsia.
Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP)
ADOLFINA CHIALO, amewata askari waliohudhuria mafunzo hayo kutunza siri
za watu wanaokwenda kwenye madawati yao kulalamikia vitendo vya ukatili
na unyanyasaji wanavyofanyiwa huku wananchi wakiombwa kutoa taarifa za
matukio hayo.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa MANYARA, SSP CHRISTOPHER FUIME, amesema
kuwa vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vya ukeketaji
watoto wa kike havikubaliki
Wakati wa Mafunzo hayo, Mtandao wa Kijinsia hapa nchini TGNP na
washirika wake wametoa msaada wa kompyuta tatu zitakazotumiwa na
waratibu wa madawati ya jinsia na watoto kwenye vituo vya polisi katika
wilaya za BABATI, KITETO na SIMANJIRO.
Home
News
Wananchi manyara waombwa kushirikiana na jeshi la polisi ili kufichua mauaji ya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment