Image
Image

Baadhi ya Wanafunzi waliotekwa na kikundi cha BOKO HARAM wako hai


Zaidi ya Wanafunzi wa Kike Hamsini waliotekwa nyara na Wanamgambo wa kiislam wa BOKO HARAM mwaka 2014 nchini NIGERIA walionekana wakiwa hai wiki Tatu zilizopita.
Mwanamke mmoja nchini humo ameliambia Shirika la Utangazaji la UINGEREZA – BBC kuwa aliwaona wasichana hao katika mji wa GWOZA kabla wanamgambo hao hawajaukimbia mji huo.
Kwa mujibu wa Mwanamke huyo ambaye naye alikua akiishi chini ya utawala wa Wanamgambo hao wa Kiislam wa BOKO HARAM, wasichana hao kwa sasa wamehifadhiwa katika nyumba moja na wamewekwa chini ya ulinzi mkali wa Wanamgambo hao.
Wanafunzi hao wa Kike ni miongoni mwa Wanafunzi wa kike zaidi ya 200 waliotekwa nyara na Wanamgambo wa Kiislam wa Boko Haram mwaka 2014 katika jimbo la CHIBOK.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment