Image
Image

News Alert: Wadau waridhia na kulifanyia kazi ombi la Rais Kikwete la kukamata na kuwarudisha mbwa mwitu ambao walikuwa wakishambulia mifugo ya wananchi wilayani Ngorongoro


Tatizo sugu na la muda mrefu la mbwamwitu  kushambulia mifugo ya wananchi katika eneo la  loliondo wilayani ngorongoro limepata ufumbuzi baada ya wadau wa uhifadhi wa ndani na  nje kukubali ombi la Mh.Rais Dr. Jakaya Kikwete la kutoa fedha kwa ajili ya kuwakamata  mbwamwitu wote walioko katika maeneo ya wananchi na kuwarudisha hifadhini.

Wadau wa nje walioanza kukubali kusaidia kazi hiyo ni pamoja shirika la Grumet Fund na  wadau wa ndani ni pamoja na shirika la hifadhi za taifa Tanzania (TANAPA) na mamlaka ya  hifadhi ya Ngorongoro,mashirika  ambayo kwa  kuanzia yameahidi kutoa jumla ya milioni  mia mbili.

Mratibu wa mradi huo wa kuwaondoa wanyama hao kwenye makazi ya watu Dr. Ernest Mjingo   na meneja wa mradi Bw.Emanuel Masenga wamesema changamoto  kubwa  inayowakabili ni  gharama kubwa ya uendeshaji hasa vitendea kazi vikwemo vifaa maalumu vya mawasiliano ya  kuratibu mwenendo wa wanyama  hao.

Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa wanyamapori (TAWIRI) inayosimamia mradi huo Dr.Simino Mduma amesema hadi sasa makundi matano yenye mbwamwitu zaidi 60 yamekamatwa  na kurejeshwa hifadhini hatua ambayo licha ya kuashiria uwepo wa wanyama hao walioko  kwenye hatari ya kutoweka ni faraja kubwa kwa sekta ya utalii.

Aliposhiriki zoezi la kurejesha kundi la tano lenye mbwamwitu 13 waliokamatwa katika  eneo la loliondo Rais wa Tanzania Mh. Dr Jakaya Kikwete aliwaomba wadau wa uhifadhi wa  nje na ndani  kusaidia zoezi hilo kuwadhibiti wanyama hao ambao licha ya kuwasabaabishia  wafugaji hasara ya kula mifugo yao wana faida kubwa katika utalii.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment