Rais uhuru kenyata wa kenya amesema amesikitishwa na magaidi walio
shambulia leo hii katika chuo kikuu cha Garissa na kuua watu 17 kujeruhi zadi
ya watu 70 na wengine kuteka nyara.
Amesema Huu ni wakati wa kila mtu nchini humo kuwa macho kama mataifa mengine ili kuendelea kukabiliana na kuwashinda maadui
wanaojipenyeza nchini humo.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametuma salam za
rambi rambi kwa familia za wale waliouawa katika shambulizi la chuo kikuu cha
Garissa kazkazini mashariki mwa Kenya.Kiongozi huyo vilevile amewahakikishia wakenya kwamba serikali yake imechukua hatua za kuwapeleka maafisa wa usalama katika eneo hilo.
Amewataka wakenya kuwa watulivu wakati huu ambapo maafisa wa usalama wanakabiliana na wapiganaji hao.
Kwaupande wake waziri wa maswala ya ndani nchini Kenya Joseph Nkaiserry amethibitisha kuwa watu 15 wameuawa huku wengine 53 wakijeruhiwa kufuatia shambulizi la alfajiri katika chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya.
miongoni mwa waliokfariki ni walinzi wawili wa mlango wa chuo hicho.
Akizungumza kutoka Garissa Nkaiserry amesema kuwa oparesheni ya kuwasaka wahalifu hao itaendelea hadi mateka wote waokolewe.
Serikali ya Kenya imemtaja Mohammed Kuno kama kuwa mshukiwa mkuu aliyepanga njama za shambulizi la chuo kikuu mjini Garissa.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari waziri wa usalama nchini Kenya Joseph Nkaiserry alitoa zawadi ya dola 53,000 kwa mtu yeyote atakayemkamata mshukiwa huyo ama kutoa habari zake.
Kuno anajulikana kama 'Gama'adhere kwa jina maarufu.
0 comments:
Post a Comment