Kuwepo kwa sheria na sera katika shule za msingi,Sekondari
na kutoa elimu kwa wanajamii hasa wazazi
na walezi kutapunguza mimba za utotoni zinazo sababisha vijana wa kike kushindwa kuendelea na masomo,kupoteza maisha yao na
watoto watakaowazaa.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa
Elimu Sekondari Wilaya ya Temeke ,
Mwalimu CHAVILA DONALD
alipokuwa akifungua mafun zo ya
elimu ya afya ya uzazi, jinsia
na stadi za maisha , kwa
wanafunzi na walimu wa shule za
Sekondari za wilaya hiyo yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Kibasila.
Mwalimu CHAVILA amesema wanafunzi ni watu muhimu wanategemewa katika familia, jamii na taifa
katika kuleta maendeleo na kupunguza umaskini.
Kwa upande wa walimu amewahimiza kuwa msaada wa kitaaluma na kijamii kwa
wanafunzi na kuhakikisha watoto wanapata elimu bora itakayowakwamua kifikra,
kijamiii na kiuchumi.
Naye Meneja Uraghibishi na Mawasiliano kutoka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo - WAMA- PHILOMENA MARIJANI ame sema mafunzo hayo ya siku tano yako chini
ya mradi wa kuzuia mimba za utotoni katika shule za sekondari unaotelelezwa na
Taasisi hiyo na Engender Health kwa
ufadhili wa Shirika la Maendeleo la watu wa Marekani.
0 comments:
Post a Comment