Zoezi la kutambua maiti linaendelea na
wakaguzi wakiendelea na zoezi la kukagua mashimo yaliyokuwa wazi huku baadhi ya
wachimbaji walionusurika katika tukio hilo wakiulalamikia ulinzi wa machimbo
hayo kuwa ndio chanzo cha tukio hilo kwakuwa tukio lilitokea mapema saa kumi na
mbili baada ya saa za kazi lakini inashangaza taarifa kupatikana saa sita za
usiku na wamedai kuwa idadi ya watu waliofukiwa na kifusi ni zaidi ya mia na
hamsini lakini serikali imeridhika na idadi ya watu kumi na tisa ambao
wameshaopolewa hadi wakati huu.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa shinyanga Justus Kamugisha
amesema watu hao walivamia mgodi baada ya muda wa kazi kuisha na kulingana na wingi
wao mgodi ulielemewa na kusababisha nguzo kuvunjika hali iliyosababisha kifusi
kuwaangukia lakini kwa jitihada za jeshi la polisi tayari wameshaopolewa watu
kumi na tisa na kumi na mbili kati yao wameshatambuliwa na tayari
wameshachukuliwa na ndugu zao tayari kwa maziko.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya kahama Bw. Benson Mwampesya amesema kwakuwa
imeonekana idadi ya vijana walioangukiwa na kifusi ni wengi zaidi ya hao
walioopolewa serikali imeamua kuomba wataalam na mitambo ya kuchimba eneo hilo
kutoka katika mgodi wa bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya acacia ili
kuharakisha zoezi la kuhakiki kuwa hakuna maiti zingine zilizonaswa katika
mashimo ya mgodi huo.




0 comments:
Post a Comment