Rais Dokta.Jakaya Kikwete
amesema serikali yake ya awamu ya nne inaendelea kujitahidi kuhakikisha kuwa
changamoto sugu zinazowakabili walimu zinapatiwa ufumbuzi na kuandaa mazingira
bora ya kuiwezesha serikali ya awamu ya tano kukamilisha ufumbuzi wa changamoto
zitakazobaki.
Dokta.Kikwete ametoa kauli
hiyo ya matumaini kwa walimu wakati akizungumza na walimu wawakilishi wa
chama cha walimu nchini wanaokutana jijini arusha.
Awali katika risala yake kwa
rais,katibu mkuu wa CWT Alhaj Yahya Msulwa aliziainisha changamoto
wanazokabiliana nazo walimu kuwa ni pamoja na maslahi duni,mazingira duni ya
kazi na sua la upandishwaji wa madaraja na marekebisho ya mishahara ambalo
anasema kikwazo kubwa kimekuwa ni watendaji hususani katika halmashauri za
wilaya.
Mkutano huo mkuu wa CWT unafanyika
sambamba na uchaguzi mkuu wa viongozi wa chama hicho katika ngazi ya kuanzia
rais na makamu wake ,katibu mkuu na naibu wake pamoja na wajumbe.
0 comments:
Post a Comment