Mmoja afariki kutokana na Ebola baada ya kukimbia hospitali Sierra Leone.
Ofisa mtendaji mkuu wa Kituo kinachoshughulikia Ebola cha Sierra Leone Bw. Pallo Conte amethibitisha kuwa, mgonjwa mmoja amefariki kutokana na virusi vya Ebola katika hospitali huko Freetown. Mgonjwa huyo alifariki wiki moja baada ya kutoroka hospitali akisaidiwa na ndugu zake na hivyo kusababisha watu 52 kuwekwa kwenye karantini kutokana na "vitendo vyake visivyowajibika".
Bw. Conte ameonya kuwa watu wanaokimbia sehemu za karantini au wanakotibiwa na wale wanaotunza wagonjwa kwa kificho "hawatanusurika na virusi vya Ebola." Amesema kifo hicho na mwingine anayeshukiwa kuambukizwa, vimefanya maendeleo yanayopatikana nchi hiyo yasimame, kwani nchi hiyo ilikuwa na rekodi ya siku nane bila kuwa na mgonjwa mpya wa Ebola.


0 comments:
Post a Comment