Image
Image

News Alert: Wanafunzi wa vyuo vikuu watoa tamko kwa tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu mkanganyiko wakati wa kupiga kura kwa watakaokuwa nje ya maeneo waliyojiandikishia.


Katika  kuelekea  uchaguzi  mkuu,umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu wa CHADEMA kupitia  baraza la vijana wa chama hicho   mkoa wa Tabora wametoa tamko la kuitaka tume ya taifa ya uchaguzi kuweka bayana namna ambavyo wanafunzi wataruhusiwa kupiga kura mahali popote walipo  kwakuwa siku ya kupiga kura  vyuo  vitakuwa vimefungwa  na wengi wao kurejea  makwao  hatua ambayo wamedai kuwa itawanyima haki  hiyo kwakuwa  si sehemu waliyojiandikishia  kupiga kura.

Wakizungumza katika ofisi za Chadema kanda ya Magharibi   mjini Tabora, viongozi wa Bavicha na Chaso,wameonesha  wasiwasi mkubwa  wa  kudai  kuanza kwa mizengwe ya  kunyimwa  haki  ya kupiga kura kutokana  na mkanganyiko  katika fomu ya maombi ya utambulisho wa mpiga kura inayotolewa  na tume ya taifa ya uchaguzi wanazotakiwa kujaza na wanavyuo,na utaratibu mzima wa zoezi la uchaguzi litavyoendeshwa  wakilinganisha na lile la  uchaguzi  mkuu   wa mwaka 2010 hasa kwa kufungwa vyuo na wanafunzi kurudi makwao  maeneo ambayo kimsingi hawakujiandikishia  katika daftari la kudumu la mpiga kura.

Katibu wa Chadema mkoa wa Tabora Bw.Alinanuswe  Edson  ameiomba serikali kulishughulukia mapema suala  hilo ambalo amedai huenda likaleta mzozo ambao pengine ukasababisha athari kubwa hususani kwa vijana.

Aidha  katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 baadhi ya wanafunzi wa vyuo  imedaiwa  kuwa  hawakupata  fursa  ya  kupiga kura ipasavyo  kutokana na  kuwepo kwa  mkanganyiko uliosababishwa na kuondoka  maeneo ambayo walijiandikishia  kupiga kura na hivyo kuleta usumbufu mkubwa katika kuteleza haki hiyo ya kimsingi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment