Deni hilo limesababisha
wabunge kutaka ufafanuzi wa kina kuhusu deni ambalo linazidi bajeti ya miradi
ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Akiwasilisha Maoni ya Kambi
ya Upinzani bungeni jana, Msemaji wa Upinzani katika wizara hiyo, Felix
Mkosamali alimtaka Dk. Mgufuli kulifafanulia Bunge madeni ambayo yamefikia Sh
bilioni 800.
Alisema katika mwaka wa fedha
2015/16, wizara hiyo imetenga bajeti ya maendeleo Sh bilioni 890.57 kwa taasisi
zilizo chini yake wakati deni ni Sh bilioni 800.
“Mheshimiwa Spika, licha ya
wizara hii kuwa na kelele na mbwembwe nyingi ukweli ni kwamba madeni ya wizara
yanazidi fedha za maendeleo tunazopitisha katika Bunge lako tukufu,” alisema
Mkosamali.
Mkosamali ambaye pia ni
Mbunge wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi), alitoa mfano kuwa bajeti ya 2014/15, wizara
ilikuwa na madeni yanayofikia Sh bilioni 760 huku bajeti ya maendeleo kwa
wizara na taasisi zake zikiwa Sh bilioni 762.
Alisema huo ni ushahidi
wizara hiyo haikuwa na fedha za maendeleo kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Kivuko Dar-Bagamoyo
Kuhusu kivuko cha Bagamoyo,
Mkosamali aliliomba Bunge kuunda tume huru ya kuchunguza ununuzi wa kivuko
hicho kwa sababu ni kibovu, licha ya kununuliwa kwa bei kubwa.
“Mheshimiwa Spika, ni jambo
la ajabu kivuko hiki kimenunuliwa kwa takribani Sh bilioni nane, kinabeba
abiria 300 kinatumia saa tatu kutoka Dar es Salaam kwenda Bagamoyo na kurudi
mara moja tu kwa siku.
“Hali hii imechangia kivuko
hiki kukosa abiria na hivyo wananchi wanaona afadhali kupanda daladala kuliko
kivuko kinachotumia saa tatu.
Alisema kambi yake imebaini
Dk. Magufuli amekuwa akiaandaa bajeti ndefu kuwachanganya wabunge huku
akiunganisha barabara zilizojengwa miaka 1980 na 1990 kama vile zimejengwa leo.
KAPUYA
Naye Makamu Mwenyekiti wa
Kamati Miundombinu, Profesa Juma Kapuya alisema wakati wanachambua utekelezaji
wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka2014/15 na makadirio ya 2015/16, walijulishwa
kuwapo madeni makubwa ya wakandarasi na wahandisi washauri wa barabara ambayo
yamekuwa yakiongezeka.
“Mheshimiwa Spika, kuendelea
kulimbikiza madeni haya kunasababisha hasara mbalimbali kwa Serikali ikiwamo
ongezeko la riba, kazi kufanyika kwa muda mrefu na wakandarasi wadogo
kufilisika,”alisema Profesa Kapuya.
Trillioni 4/- Dar
Trillioni 4/- Dar
Awali akiwasilisha bungeni
mpango wa makadirio ya mapato na matumizi wizara yake kwa mwaka 2015/16, Waziri
wa Ujenzi Dk. John Magufuli alisema aliisema miradi yote iliyopangwa
kutekelezwa na wizara yake itakapokamilika itagharimu Sh trilioni 4.394.
Waziri alisema sehemu ya
barabara ya Dar es Salaam –Chalinze imepangwa kujengwa kwa kiwango cha barabara
sita na itatekelezwa kwa utaratibu wa ubia kati ya Serikali na sekta binafsi
(PPP).
“Mheshimiwa Spika, suala la
kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam ni suala mtambuka
linalohusisha wizara na mamlaka mbalimbali zikiwamo halmashauri za Jiji.
“Maandalizi ya ujenzi
barabara ya njia sita ya Dar es Salaam – Chalinze – Morogoro (kilomita 200)
sehemu ya Dar es Salaam – Chalinze (kilomomita 100) imepangwa kujengwa kwa
kiwango cha “Expressway”. Maandalizi ya mradi huu utakaotekelezwa kwa utaratibu
wa ubia baina ya Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partnership – PPP)
yameanza.
Kuhusu ujenzi wa daraja jipya
la Selander, Dk. Magufuli alisema lengo kuu ni kupunguza msongamano wa magari
katika eneo la Selander na Serikali ya Korea Kusini imekubali kuipatia Tanzania
mkopo wa masharti nafuu kwa ajili ya ujenzi huo.
Alisema daraja hilo pamoja na
barabara zake za maingilio litakuwa na urefu wa kilomita 7.2 na litaanzia eneo
la Koko Beach kupitia Kenyatta Drive na kuingia baharini na kisha kuungana na
barabara ya Barack Obama eneo la Hospitali ya Aghakan na utagharimu Sh bilioni
197.5.
Magufuli alisema katika
kipindi cha miaka 10 Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete,
imejenga barabara zenye urefu wa zaidi ya kilomita 17,762.
Wabunge
Baadhi ya wabunge
wameshangazwa na hatua ya Serikali kutenga bajeti ya Wizara ya Ujenzi isiyo
halisi huku wengine wakipatwa na wasiwasi iwapo miradi mipya ya barabara
itatekelezwa mwaka huu.
Katika michango yao bungeni
jana, wabunge hao walisema wizara hiyo imezidiwa na madeni ya wakandarasi
kutokana na Serikali kushindwa kutoa fedha na nyingine kutumiwa vibaya.
Mbatia
Akichangia bajeti hiyo, Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), alisema bajeti hiyo ni kiini macho kutokana na kuzongwa na madeni makubwa ya wakandarasi.
Akichangia bajeti hiyo, Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), alisema bajeti hiyo ni kiini macho kutokana na kuzongwa na madeni makubwa ya wakandarasi.
“Wizara hii inadaiwa na
wakandarasi deni la Sh bilioni 850 hadi bilioni 900 kuliko fedha zinazoombwa,
hivi nyinyi mtafanyaje kazi kwa bajeti hii?
“Mwaka jana mfuko wa barabara
ulitengewa Sh bilioni 600, lakini fedha hukupewa zote… Serikali hapa imevunja
Katiba, ibara ya 135 inaeleza kuwa fedha zinazotengwa kwa kazi fulani zinapaswa
kutumika kwa kazi husika.
“Wapo wakandarasi wanne
wamepoteza maisha kutokana na kutolipwa madeni yao, hivi kweli hadi imefikia
mahali wananchi wetu wanapoteza maisha kwa sababu ya madeni ya Serikali,”
alisema.
Msigwa
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji
Peter Msigwa (Chadema) alisema mkoani Iringa pekee wakandarasi wanaidai
Serikali mabilioni ya shilingi jambo ambalo limeathiri hadi maisha ya mama
lishe.
“Mimi nashangaa, sisi wabunge
tunakwenda nje ya nchi tunaona barabara za wenzetu. Hizi barabara za wenzetu ni
sawa na hizi za kwetu? Mbona tunajitoa fahamu, tuache kujikombakomba kwa vitu
visivyokuwa na maana.
“Dar es Salaam ni jiji la
mfano lakini miaka 30 imepita jiji halina master plan (mipango miji), eti
wabunge wengine wanalinganisha barabara zetu na zile za Dubai, jamani tuache
hizo.
“Hizi barabara zetu ni za
kwenda migombani, huwezi kulinganisha barabara hizi na zile tunazoziona katika
nchi za wenzetu, huwezi kujisifia kwa barabara ambazo ni disposable (za muda),”
alisema.
Msigwa aliishangaa Serikali
kununua Kivuko cha Bagamoto Dar es Salaam kwa gharama kubwa huku kikijiendesha
kwa hasara.
“Kwa kivuko hiki mtu anaweza
kwenda Zanzibar kutoka Dar es Salaam na kurudi mtu aliyetoka Bagamoyo hajafika
Dar es Salaam. Kivuko kinatumia saa tatu nauli Sh 1500 kwa safari moja Serikali
inapata Sh 450, 000 wakati mafuta yanayotumika katika kivuko hicho ni Sh
milioni 2.4 waziri mnafanya kitu gani?” alihoji.
Mkosamali
Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi), aliwashangaa wabunge wanaosifia Serikali badala ya kutimiza wajibu wao wa kuisimamia Serikali.
Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi), aliwashangaa wabunge wanaosifia Serikali badala ya kutimiza wajibu wao wa kuisimamia Serikali.
“Kuna mbunge mmoja alisimama
hapa akaisifia Serikali, yaani fedha zinapunguzwa halafu mbunge anakuja hapa
anasifia. Mwaka jana Serikali iliahidi kutoa Sh bilioni 10 Kigoma katika bajeti
hii fedha iliyotengwa ni Sh bilioni 7, mtu anasifia,”alisema.
Sendeka
Mbunge wa Simanjiro,
Christopher ole Sendeka (CCM), alisema anawashangaa wabunge ambao
wanaishambulia Serikali kutokana na bajeti ndogo badala ya kushauri namna ya
kupata fedha.
“Kule kwangu Simanjiro hakuna
hata hatua moja ya lami, acha kilomita moja, hatua moja hakuna lakini hii
haiondoi ukweli kwamba Serikali imejitahidi katika sekta ya ujenzi.
“Zipo changamoto, madeni ni
mengi, fedha haziendi hivi mnategemea Maguli atafanya kitu gani? Barabara
haziwezi kujengwa kwa kupiga kelele tuunganishe nguvu sote kwa umoja watu,”
alisema.
Mtemvu
Mbunge wa Temeke, Abbas
Mtemvu (CCM), alisema haungi mkono bajeti hiyo kutokana na tatizo la msongamano
katika jiji la Dar es Salaam.
“Wananchi wa Temeke
wamenituma nisiunge mkono bajeti hii na sababu ni moja tu, msongamano katika
jiji la Dar es Salaam, hali ni mbaya, inatisha inatia huruma.
“Leo hii Dar es Salaam mtu
anatumia saa sita kutoka kazini kwenda nyumbani kwake. Mheshimiwa Magufuli juzi
ulisema asilimia 65 ya mapato inatoka Dar es Salaam, lakini hutuwatendei haki
watu wa Dar es Salaam.
“Nakuomba mheshimiwa muda
uliobaki ni mfupi tunaomba sana tusaidie tupate fedha kwa ajili ya barabara za
ringroad (barabara za pete). Barabara nyingi Dar es Salaam hivi sasa hazipitiki
kutokana na mvua na wakandarasi wamelipwa,” alisema.
0 comments:
Post a Comment