Ripoti hiyo iliyowasilishwa
jana ilibainisha kuwa kwa matukio ya vifo vinavyotokana na imani za ushirikina
yameongezeka mwaka 2010 hadi 2014 kutoka watu 2,583 hadi 2,936.
Aidha, ripoti hiyo inaonyesha kulitokea ajali za barabarani 21,791 ambazo
zilisababisha vifo vya 3,437.
Ripoti ya LHRC iliyotolewa na
Jaji mstaafu, Amir Manento, inasema kwamba ajali za barabarani zilitokea katika
miji mikubwa.
Aidha, ripoti hiyo imesema
watoto wa kike 1,302 walikeketwa katika kipindi cha mwaka 2014 katika
mikoa ya Singida na Mara, huku wanawake 2,878 wakifanyiwa vitendo vya ubakaji
wengi wao wakiwa ni watoto.
Ripoti hiyo ya LHRC ambayo
hutolewa kila mwaka imesema mauji ya raia yanayofanywa na vyombo vya dola
yamepungua kwa mwaka 2014.
Ripoti ya ukeketaji kwa mwaka
2009 ilionyesha kwamba wasichana 371 walibakwa wakati mauaji yaliyotokana na
ushirikina yalikuwa 2,583.
Mauaji ya polisi katika Mkoa
wa Pwani mwaka jana yametajwa katika ripoti hiyo kwamba yameleta madhara kwa
kuwa chombo hicho ndicho kinacholinda amani hapa.
Kadhalika, Jaji Manento
alisema ikiwa miswada ya habari ya haki ya kupata taarifa na huduma za vyombo
vya habari itasainiwa na Rais ili iwe sheria, itazika rasmi demokrasia nchini.
Jaji Manento alisema bado
kuna safari ndefu kutekelezwa nchini ikiwamo kuminya uhuru wa kuwapo mgombea
huru na rushwa kushamiri katika katika chaguzi, mambo yaliyopigiwa kelele na
LHRC.
“Kutamka neno demokrasia na
haki za binadamu bila kuzisimamia na kuzitekeleza, ni kazi bure,” alisema Jaji
Manento wakati akiitangaza ripoti hiyo ya kila mwaka.
Ripoti hiyo ya mwaka 2014 ya
LHRC inasema uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwishoni mwa jana,
ulivurugwa kutokana na wasimamizi wa uchaguzi kuchelewa kufika vituoni na
vurugu mbalimbali vituoni.
Alisema suala la demokrasia
limekuwa likitamkwa mdomoni, lakini usimamizi na utekelezaji wake bado
umeendelea kuwa mgumu.
Aidha, LHRC kimetabiri kwamba
uchaguzi mkuu kwa mwaka huu utakuwa mgumu kwa sababu vyama vya upinzani
vimeimarika na Chama Cha Mapinduzi (CCM), nacho kimejiimarisha.
Akizungumza kabla ya kuzindua
ripoti hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Hellen Kijo-Bisimba, aliitaka
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), irekebisha dosari mbalimbali zilizojitokeza
katika uandikishaji wa wapigakura kupitia mfumo wa BVR.
Aidha, Dk. Bisimba aliiomba
serikali kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki mbalimbali zikiwamo za afya,
elimu, kulindwa, kuwa huru kuchagua viongozi wa kisiasa, kushiriki katika siasa
na kuachana na aina yoyote inayolenga kukandamiza haki za binadamu.
0 comments:
Post a Comment