Image
Image

Wapinzani Burundi: Maandamano lazima yaendelezwe.


Viongozi wa upinzani nchini Burundi wamewataka wananchi wa nchi hiyo kuendeleza maandamano ya kupinga hatua ya Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza ya kugombea kwa muhula wa tatu. 
Viongozi muhimu wa upinzani nchini Burundi walisema hayo jana katika mkusanyiko wa wananchi na kuwataka waondokane na woga na kuendeleza maandamano licha ya kukabiliwa na ukandamizaji unaofanywa na vyombo vya usalama vya nchi hiyo. Dieudonné Bashirahishize, mmoja wa wawakilishi wa jumuiya za kiaraia nchini Burundi ameashiria katika mkusanyiko huo juu ya kuuawa raia 20 hadi sasa na kuwataka wananchi kutolegeza kamba na kupuuza tahadhari iliyotolewa na Baraza la Usalama wa Taifa la Burundi. 
Jana makumi ya vijana waliandamana katika viunga vya mji mkuu Bujumbura kupinga hatua ya Rais Nkurunziza ya kutangaza nia yake ya kugombea katika uchaguzi ujao wakisema inapingana na Katiba na ni kinyume kabisa na makubaliano ya Arusha. Wakati huo huo, duru za habari zinasema kuwa, tume ya kusimamia uchaguzi nchini humo, imekubali kuakhirisha uchaguzi wa bunge uliokuwa umepangwa kufanyika terehe 26 ya mwezi huu kwa muda wa wiki moja mbele.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment