MSHINDI wa tuzo ya
Mtayarishaji Bora wa Wimbo wa Mwaka- Bongo Fleva katika Kili 2015, Nahreel
amesema kuwa nyimbo za msanii Diamond na Joh Makini alizotengeneza zimempa
zimemuunganisha na wasanii wakubwa wa Nigeria na sehemu nyingine.
Akizungumza Dar es Salaam Naheel
alisema yeye ndiye mtozi wa wimbo wa kushirikiana mpya waa Diamond na Falavour
wa Nigeria ‘Nana’ pamoja na ‘Nusu nusu’ ya Joh Makini ambazo video zake
alizifanya Afrika Kusini na zinachezwa na vituo kama Trace Urban, MTV Base na
Sound City na nyingine.
Mtozi huyo wa The Industry na
msanii NavyKenzo alisema kuwa ubora wa midundo ya ngoma hizo umemvutia
staa wa Nigeria, Yemi Alade ambaye ameonesha nia ya kutaka kufanya naye kazi.
“Tangu nilipotengeneza wimbo
wa Nana ya Diamond na Nusu ya Joh Makini nimeanza kupokea mawasiliano kutoka
Nigeria na sehemu mbalimbali, kwa mfano Vanessa Mdee pia ametoka kuniambia kuwa
Yemi Alade anataka kufanya kazi na mimi chini ya The Industry Studio kwa hiyo
mashabiki wa Naheel wakae tayari kwa muziki mzuri,”alisema Naheel.
0 comments:
Post a Comment