Waziri wa ushirikiano wa afrika ya mashariki Mh.
Harrison Mwakyembe ameeleza kusikitishwa na kufedheheshwa na tabia ya baadhi ya
watu kutokuwa majasiri na kutumia majina ya watu wengine kutoa maoni ama
misimamo yao kwenye mitandao ya kijamii ambapo ametoa mfano wa jina lake kutumika kumchafua Mh. Edward Lowasa kuhusu
RICHMOND.
Amesema kuwa wapo watu
wanaojaribu kutengeneza mambo kusudi kuchafua jina lake hali ambayo haikubaliki
hata kidogo huku akisema kwamba suala la Richmond lilishakwisha muda mrefu
kwani kazi yake ilikuwa nikuchunguza na kuleta ripoti hivyo anashangaa watu hao
wanaoanza kutunga mambo na kusambaza.
Anasema yeye suala lolote analo
lishughulikia huwa anajua namna ya kuklikusanyia taarifa na hakuna ubishi huo
na mwisho wasiku likaleta majibu mazuri hivyo mtu ambaye anajisikia kukaa tu
chini na kutunga mambo na kusambaza hiyo sawa nay eye anasema limemfedhehesha
mno mno kwa kuwa halina ukweli.
Kauli yake hii ameitoa wakati wa
mahojiano yake na baadhi ya vituo vya Radio na Runginga(TV) jijini Dar es
Salaam uliojikita kufahamu ukweli wa taarifa hizo ambazo zimekuwa zikisambaa
ambapo Mh.Mwakyembe amekanusha kuhusika na kuongeza kuwa suala hilo si lake bali ni
maamuzi ya Bunge na kwamba suala la Richmond lilifungwa miaka saba iliyopita.
Amesema kuhusiana na taarifa hizo zinazo sambaa katika
mitandao ya kijamii na hata wakati mwingine kuchapishwa katika baadhi ya
magazeti bila kumuhoji hali ambayo inamfanya wakati mwingine kupokea simu kwa
watu mbali mbali na wakimuuliza vipi mbona umetumia maneno makali katika
taarifa zako katika vyombo vya habari amesema hata yeye amebaki akishangaa
kutokana na kwamba taarifa hizo kwake ni mpya.
Pia Mh.Mwakyembe amesema atahakikisha mara baada ya
uchunguzi kukamilika kuweza kuchapisha picha zao katika vyombo vya habari ili
watanzania wawatambue,amesema hadi sasa wameshawapata wa nne katika uchunguzi
wa awali hivyo watachunguza hadi kupatikana kinara mkuu wa usambazaji wa
taarifa hizi.
0 comments:
Post a Comment