Uamuzi huo umefikiwa jana jijini Dar es Salaam na
kusomwa na Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Richard Sezibera kwa niaba ya wakuu wa nchi
za Afrika Mashariki, akisema utasaidia kupunguza vurugu zilizokuwa zikiendelea
nchini humo.
Burundi ilikuwa imepanga kufanya uchaguzi wa wabunge
wiki ijayo na wa rais Juni 26.
Uamuzi mwingine umezitaka nchi za EAC kuisaidia
Burundi kurejesha wananchi wake waliokuwa wamekimbilia huko kutokana na
machafuko yaliyotokea.
Pia EAC imetoa wito kwa pande mbili zinazohasimiana
kukaa meza moja na kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani ili kudumisha
demokrasia nchini humo.
Wakati mkutano huo ukiendelea ripoti zinasema kuwa
ofisa mmoja wa Tume ya Uchaguzi ameiambia redio moja ya Ufaransa kuwa ofisa
mwenzake, Spes Caritas Ndironkeye hajulikani alipo tangu Ijumaa.
Hata hivyo duru zinaeleza kuwa huenda ofisa mwingine
akajiondoa na hivyo kusababisha shughuli za tume hiyo kuzorota.
0 comments:
Post a Comment